Tuesday, March 7, 2023

Saturday, March 4, 2023

MSHINDI WA SITA NA WATANO MASHINDANO YA BENDI MWAKA 1988


 HAKIKA kumekuwa na utata kuhusu mashindano ninayoyaongelea ni ya mwaka gani. Mashindano ya bendi ambayo yalifahamika kama Top Ten Show yalifanyika mara mbili.  Kwa mara ya jkwanza yalifanyika mwaka 1988 na mara ya pili yakafanyika kuanzia tarehe 29 Julai 1989 na kumalizika tarehe 25 Novemba mwaka 1989. 

Katika mashindano ya kwanza kila bendi ilipewa uhuuru wa kuchagua nyimbo moja  ambayo ishiriki katika mashindano hayo. Katika mashindano ya pili bendi zilipewa nafasi tatu, ya kwanza ni wimbo wowote ambao bendi ingechagua nafasi ya pili ilikuwa ni wimbo wenye'tuni' asili na wimbo wa tatu ulipea jina Afrika Nakulilia.

Mashindano ambayo mnayasikia hapa ni ya shindano la kwanza la 1988. Nategemea wote tunaenda sawa sasa


Wednesday, March 1, 2023

HOTUBA YA DR ALEX KHALID KWENYE FAINALI YA TOP TEN SHOW 1988, UTADHANI ANAONGELEA HALI YA LEO (Part 1)

MWISHONI  mwa mwaka 1989 na mwanzoni mwa 1990 lilifanyika shindano kubwa la kupata nyimbo bora lililojulikana kama Top Ten Show. Bendi nchi nzima zilishiriki, RTD ilipita mikoa mbalimbali na kurekodi maonyesho 'live' ya bendi ambazo zilikuwa ndani ya mashindano hayo. Hatimae siku ya kilele ilifika, sasa hebu sikiliza hapa uchambuzi wa mwenyekiti wa jopo la majaji wa shindano lile Marehemu Balozi Dr Alex Khalid akichambua yaliyojiri, utadhani anaongelea muziki wa dansi leo, miaka 42 baadae. 

Je ina maana bendi bado ziko palepale zilipokuwa 1988?

 Toa maoni yako



Tuesday, January 10, 2023

MAQUIS ORIGINAL WAJIKUSANYA TAYARI KWA MAONYESHO MAKUBWA MAWILI YA PAMOJA

MAMBO MATAMU YAJA
BENDI kongwe iliyokuwa maarufu sana, Maquis Original itauanza mwaka huu kwa kufanya maonyesho mawili makubwa ya kumbukizi ya enzi zake. Maquis Original awali ilikuwa ikiitwa Maquis du Zaire wakati ikiingia nchini Tanzania kwa mara ya kwanza, ilikuwa ikitokea  mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakati huo nchi hiyo ikiitwa Zaire.
 Baada ya kuwasili Tanzania, haikupita muda mrefu bendi ikawa moja ya bendi tishio nchini. Nyimbo za bendi hii hata zile ilizo rekodi mwanzoni baada ya kuingia nchini bado ni nyimbo pendwa kwa waliokuweko enzi hizo na hata ambao wamezaliwa miaka mingi baada ya bendi kuwa imepotea katika ulimwengu wa muziki. Uamuzi wa wanamuziki wa bendi hii kujikusanya na kufanya maonyesho yao hakika ni faraja kubwa kwa wapenzi wa bendi hii. Bendi itafanya maonyesho mawili. Onyesho la kwanza litakuwa tarehe 21 Januari 2023 katika ukumbi wa Break Point Makumbusho na tarehe 27 January katika ukumbi wa Royal Village Dodoma

Hebu tukumbuke enzi hizo kwa kuangalia tangazo la dansi la Orchestra Maquis miaka hiyo ambalo nina uhakika litaleta kumbukumbu kwa wapenzi wa Maquis wa enzi hizo za Mtindo wa Telemka Chekecha Scania LBT III, wakati huo gari za Scania ndizo zilikuwa maarufu nchini na Scania LBT III ilikuwa gari yenye saiz kubwa kuliko zote, na ndio yenye kusifika zaidi. Maquis walikuwa na ufadhili wa kampuni hiyo ya magari, ukumbi wa nyumbani wa bendi hii wakati huo ulikuwa ukumbi wa White House uliokuwa Ubungo. Karibuni tena wapenzi wa White House mchangie, mambo yalikuwa mazito chini ya uongozi wa Chinyama Chiyaza ambae alikuwa mpiga Saxophone katika bendi. Wakati huu Maquis ilikuwa na maendeleo makubwa sana ya kuwa na mashamba, magari, matrekta na hata kuwa na Kota zake pale Sinza Palestina. Hebu angalia majina ya wanamuziki waliokuwa kwenye bendi hiyo, wote walikuwa miamba ya muziki.

MWAKA MPYA NGUVU MPYA


 

Thursday, December 22, 2022

WASIFU WA MAREHEMU RAMADHANI KINGUTI - KINGUTI SYSTEM

 


Marehemu Ramadhan Maulid Kinguti maarufu kama Kinguti System ni mzaliwa Ujiji, Kigoma. Alikuwa mtu aliyependa sana utani na ucheshi.

Bendi yake ya kwanza aliyojiunga mwaka 1977, ilikuwa Super Kibisa iliyokuwa na makao yake makuu Kigoma. Super Kibisa  ni bendi iliyoanzishwa mwaka 1968 pale Kigoma. Mwaka 1977 kiongozi wa bendi alikuwa Mlolwa Mussa Mahango ambaye alikuwa ni binamu yake Ramadhani Kinguti, na  hivyo ikawa rahisi  kwake kujiunga na bendi ile. Super Kibisa ilikuwa mali ya watu watatu, Gollo Saidi, Haruna Mahepe, na Maulidi. Katika bendi ya Super Kibisa, kipaji cha utunzi cha Kinguti kilianza  kujitokeza mapema na aliweza kutunga nyimbo kadhaa kama vile Kazi ni uhai, Mapenzi tabu,na Zaina.

Miaka miwili baadae, 1979, Kinguti alichukuliwa na Ahmed Sululu ambae alikua Katibu wa bendi ya  Dodoma International na kuhamia Dodoma. Dodoma International ilimchukua Kinguti ili kujaza nafasi ya Shaaban Dede ambaye alikuwa kahama bendi hiyo na kuhamia JUWATA.

Alipofika Dodoma international , Kinguti  alikutana kwa mara ya kwanza na mpiga gitaa mahiri marehemu Kassim Rashid. Kinguti aliiacha Dodoma International Orchestra na kujiunga na  Orchestra Makassy ambapo wakati huo walikuweko wanamuziki akina Marehemu Masiya Radi, mwimbaji  Mkongo ambaye alifariki kwa kukanyagwa na daladala maeneo ya Kinondoni Mbuyuni. Baadhi ya wanamuziki wengine ambao Kinguti alikuwa nao alipokuwa Orchestra Makassy walikuwa marehemu  Remmy Ongala, marehemu Andy Swebe, Keppy Kiombile, John Kitime, marehemu Issa Nundu, marehemu Kyanga Songa, Choyo Godjero na wengineo, pia alikuweko marehemu Aimala Mbutu kwenye solo, na Kassim Mganga (babake wa mwanamuziki wa Bongo flava Kassim Mganga-Milionea wa Mahaba) kwenye rhythm, na wengine wengi.  Kwa kipindi fulani muda huu Kinguti akiwa na wenzake chini ya Mzee Makassy wakafanya ziara ndefu nchini Kenya, kati ya waliokuwepo katika safari hiyo ni Nico Makoli,  Keppy Kiombile, Andy Swebe, Mzee Aimala Mbutu, Mzee Liston na wengine wengi akiwemo Mzee makassy mwenyewe.

1986 alijiunga Afrisongoma chini ya Lovy Longomba, hapa alitunga nyimbo kadhaa kama Pesa ni maua, Amana mpenzi, Estah Usituchonganishe, waimbaji wakati huo walikuwa Kinguti, marehemu Lovy Longomba  na Anania Ngoliga, kwenye solo alikuweko marehemu Kassim Mponda, na rhythm Maneno Uvuruge. Kwa muda mfupi alikuwa DDC Mlimani Park, na hapa akatunga kile kibao maarufu Visa vya mwenye nyumba, ambapo aliimba na Hassan Bitchuka, Francis Lubua, Hussein Jumbe na Benno Villa. Mwaka 1989 alikuwa moja ya wanamuziki waanzilishi wa Bicco Stars Band akiwa na Mafumu Bilali, Asia Darwesh, Andy Swebe, Mzee Aimala Mbutu, walitikisa na vibao kama Muuza chips, Leyla, Magreth maggie, Kitambaa cha kichwa, Nyumba ya kifahari, na nyingine nyingi tu. 1999 alijiunga na kilimanjaro Connection, alikaa bendi hii iliyokuwa chini ya Kanku Kelly kwa miaka miwili kisha kuanzisha bendi akiwa na Hassan Shaw, bendi iliyoitwa The Jambo Survivors ambayo wengi hapa Tanzania wataikumbuka kwa kibao cha Maproso. Bendi ya Jambo Survivors ikiwa bado na Ramadhan Kinguti na Hassan Shaw, kwa miaka kadhaa ikahamia Thailand. Baada ya kurudi Thailand afya ya Kinguti ilikuwa na migogoro mingi hivyo hakurudi tena kwenye muziki na muda mwingi alikuwa Dar es Salaam kisha Kigoma.

Ramadhani Kinguti amefariki tarehe 21 Disemba 2022 katika hospitali ya Maweni Kigoma, na mazishi ni tarehe 22 Disemba 2022 hapohapo Kigoma

Mungu amlaze Pema.

Sunday, December 18, 2022

TWO DAYS AFTER REMMY ONGALA DIED, HIS DRUMMER FOLLOWED HIM

The late Abou Semhando.

It was around three o'clock at night, on Saturday 18 December 2010, when I got a call from veteran musician Luiza Nyoni, she was crying and told me that there had been an accident and Abou Semahando who was on a motorcycle had been hit by a car and had died, the accident had happened in Mbezi Tanki Bovu. I woke up and went to the accident site and alas the information was true. I found Abou's motorcycle had already been loaded in a police car and the car that had hit him was in the ditch.  

In the accident, a van hit him in the back while he was on his motorcycle on his way home after a performance by his band, somewhere in  Africana area. According to his fellow musicians, Abou last played the drums for the second last song and decided to go home, minutes later got into a fatal accident. The strange thing is that Abou on his motorcycle led the funeral procession of Dr. Remmy Ongala just two days before his death..

The car involved in the accident

Abou's mangaled
 motorcycle

The car 

Abou Semhando first on right with a red shirt, in a group photo with fellow musicians during the Dr Remmy's funeral ceremony

Timetable for funeral arrangements for the late Abou Semhando (Baba Diana), musician and manager of the African Stars Band-Twanga Pepeta

• Saturday 18/12/2010-friends and relatives gathered at the home of the deceased, Mwananyamala Kisiwani (Ngilangwa) to offer condolences and console the bereaved.

• Sunday 19/12/2010- 5:00 AM.  Dawn prayers at  Muhimbili mosque, after the prayer the mourners would travel to Kibanda, Muheza ready for the funeral.

• Immediately after lunch the body would be moved to the Muheza mosque and after prayer the body would be taken to the cemetery for burial.

• Mourners would return to Dar es Salaam after the burial.

Some notable things:

1.19/12/2010 was  the day his eldest daughter was to be married

2. He had written to the management of the Band to give him a month's leave because he wanted not to be on stage for a while. It is the first time he wrote a letter requesting leave

3. The ringtone he put on his phone is the song by Njohole Jazz Band - this band's musicians almost all died together in a bad car accident.


Standing from left to right -.Remmy Ongala, Abuu Semhando,Kasaloo Kyanga, Fan Fan they are all deceased.

I first met Abou Semhando around 1979, we were both working with Printpak Tanzania Ltd, he was in typesetting department I was a proofreader. At the time he was with Sola TV Band I was with the Oshekas Band, but I would honestly say we were not close in any way. In 1989 I joined the Vijana Jazz band he was the band's second in command and we became quite close after. In his lifetime Abou was a member of several bands including Sola TV, Vijana Jazz, Diamond Sound and Super Matimila.
In the evening after DR Remmy's burial,
 Abou Semhando and Cosmas Chidumule, a veteran musician who was once also a member of Super Matimila Band under Dr Remmy Ongala,Semhando were joking about who would follow after the death of their colleague.

Abou Semhando : You will follow and back his songs like you always did.

Cosmas Chidumule: No way, you should follow him after all you were his drummer for a longer period.

Two days later it was a joke no more Abou went on to join his comrade

MAY GOD FORGIVE THEIR SHORTCOMINGS 

AMEN


ABOU SEMHANDO ALIFARIKI SIKU MBILI BAADA YA KUONGOZA MSAFARA WA KUMZIKA DR REMMY

MarehemuAbou Semhando.

Ilikuwa ni mida ya saa tisa usiku, alfajiri ya Jumamosi 18 December 2010, nilipopigiwa simu na mwanamuziki mkongwe Luiza Nyoni, alikuwa analia akanambia kumetokea ajali na Abou Semhando aliyekuwa kwenye pikipiki amegongwa na gari na amefariki, ajali ile ilikuwa imetokea maeneo ya Mbezi Tanki bovu. Niliamka na kuelekea eneo la ajali na hakika taarifa ile ilikuwa ni ya ukweli. Nilikuta pikipiki ya Abou imepakiwa katika gari la polisi na gari iliyomgonga ikiwa kwenye mtaro. Abou ambaye kati bendi alizopigia ni pamoja na Sola TV, Vijana Jazz, Diamond Sound na Super Matimila kweli alikuwa amefariki..
Katika ajali hiyo gari aina ya benzi ilimgonga nyuma akiwa katika pikipiki yake wakati akitoka kupiga mziki maeneo ya Africana. Kwa maelezo ya wanamuziki wenzake Abou alipiga drums nyimbo ya pili toka mwisho na baada ya hapo kuamua kuelekea nyumbani ambapo ndipo alipokutana na ajali hiyo. Jambo la kusikisha pia ni kuwa Abou aakiwa na pikipiki yake ndiye aliyeongoza msafara wa mazishi ya Dr. Remmy Ongala siku mbili tu kabla kifo chake.
Gari lililohusika katika ajali

Pikipiki ya Abou

Gari lililohusika katika  ajali hiyo

Abou Semhando wa kwanza kulia akiwa na miwani kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Remmy Ongala siku mbili kabla ya kifo chake. 

Ratiba ya  Mazishi ya mwanamuziki na na meneja wa Bendi ya African Stars-Twanga Pepeta  Marehemu Abou Ally Semhando “BABA DIANA”

         Jumamosi 18/12/2010-ndugu na jamaa kukusanyika nyumbani kwa marehemu, Mwananyamala Kisiwani(Ngilangwa) kwa ajili ya kutoa pole na kuwafariji wafiwa.
         Jumapili 19/12/2010-Saa 11 Swala ya alfajiri katika msikiti wa Muhimbili, baada ya swala waombolezaji kuingia katika magari na kuelekea kijiji cha Kibanda, Muheza tayari kwa mazishi.
         Mara baada ya chakula cha mchana mwili kupelekwa msikiti wa Muheza nabaada ya swala mwili kupelekwa makaburini kwa maziko.
         Waombolezaji watarejea Dar es Salaam baada ya maziko.
1.19/12/2010 ni siku aliyokuwa amuoze binti yake wa kwanza
2. Alikuwa ameuandikia uongozi wa Bendi kuwa umpe likizo ya mwezi kwani alitaka asiweko katika jukwaa kwa kipindi. Ni mara ya kwanza yeye kuandika barua ya kuomba likizo
3. Katika simu yake ringtone aliyoiweka ni ya wimbo wa Njohole Jazz Band- bendi hii wanamuziki wake karibu wote walikufa pamoja katika ajali mbaya ya gari.

Waliosimama..Remmy Ongala, Abuu Semhando,Kasaloo Kyanga, Fan Fan wote wamekwisha fariki.

Abou Semhando alikuwa mpiga drum wa Remmy Ongala enzi za Super Matimila na mtindo wao wa Talakaka. 1981. 
Mara baada ya mazishi ya Dokta Remmy, Abou Semhando na Cosmas Chidumule walikuwa wakitaniana, kuwa nani atakaefuata baada ya kifo cha mwenzao,
Abou Semhando : Utafuata wewe ukawe unamsaidia kuimba.
Cosmas Chidumule: Mi sitaki utaenda wewe  mpiga drum wake.
Siku mbili baadae Mungu akapitisha uamuzi wake.

MUNGU WASAMEHE MAPUNGUFU YAO NA KUWALAZA PEMA 
AMEN

Thursday, December 15, 2022

MUSICIANS WHO DIED IN DECEMBER

 

tHE LATE ANDY SWEBE

Many people believe that the end of the year tends to be characterized by many shocking tragedies, it seems this is true in the community of Tanzanian musicians. Here are some of the tragedies that befell the music industry in the month of December.

Let me start with the night of December 12, 2010, that night Ramadhani Mtoro Ongala, a famous musician also known as Dr. Remmy Ongala died. Remmy died at the Regency Hospital in Dar es Salaam. In his lifetime Remmy Ongala went through several bands after entering Tanzania from Congo. He arrived in the country and joined the Orchestra Makassy band, a band led by Mzee Makassy whom Remmy used to identify as his uncle. Remmy left Orchestra Makassy and joined a band based in Songea called Super Matimila, for a short time he returned to Orchestra Makassy where at that time I was lucky to be one of the musicians in the band, and on the lineup there was also the great Mosese Fan Fan who is now also deceased.

Dr Remmy again returned to Matimila where he stayed for a long time with the band that identified itself as playing the Bongo Beat style. But eventually Dr Remmy left dance music and started singing gospel music until death. Dr Remmy was buried on Thursday 16th  December 2010 in the Sinza cemetery, not far from an area named after him, 'Sinza kwa Remmy'.  On the eve of Dr Remmy's burial, various musicians gathered at Dr Remmy's house and played music throughout the night to bid farewell to their comrade. Just two days after Dr. Remmy's funeral, another musician who was riding a motorcycle that led the procession to the cemetery to bury Dr. Remmy had a fatal accident, he was hit by a car and died on the spot, he was returning home after his music gig, it was Saturday 18 December 2010.

 The musician was Abou Semuhando also known as Lokasa or Baba Diana. Abou was a drummer for many years and was with the Super Matimila at the same time as Dr Remmy. Other bands that Abou played for include Sola TV, Vijana Jazz and Diamond Sound. Abou was buried at his home village in  Kibanda, Muheza. The saddest thing is that, on the day of his death, Abou’s eldest daughter was getting married. Abou had also already written to the management of his band to ask for a leave because he wanted to rest for a while.

Another December death occurred at dawn on 28 December 2011 at the Marie Stoppes Mwenge hospital in Dar es Salaam. The talented bass guitarist Andisye Swebe, better known as Andy Swebe, suffered from an asthma attack at night , he was  rushed  to the hospital, but  Andy died. Andy started learning to play the guitar from David Mussa of Safari Trippers, after that he played in a small band called Oshekas until he moved to Morogoro where he was employed by a leather factory. One day Mzee Makassy's band had a gig in Morogoro and when he was invited on stage to play a bit, he pleased Mzee Makassy so much that he asked him to join the band, that was the beginning of Andy's long journey in music, later he went through Lovy Longomba's Afriso Ngoma band, at that time with Kassim Mponda, Raymond Thomas, Seif Lengwe, Sololo wa Imani, John Maida, Ramadhani Kinguti, Kalamazoo and others, then he moved to MK Group, later he moved to Bicco Stars, and the journey continued until he and Mafumu Bilali started the African Beats Band.  He later moved to the Kilimanjaro Connection band under Kanku Kelly and they toured several countries for several years with this band. Andy was a freelance musician without a band when death took him.

On December 15, 2014, veteran musician Shem Karenga died. Shem Karenga died at Amana Hospital and was buried at Kisutu Cemetery. Mzee Shem went through several bands including Lake Tanganyika Jazz of Kigoma, Tabora Jazz, and MK Beats and finally Tabora Jazz Stars, he was a very talented soloist, singer and composer.

Let me finish the article by remembering the musician whom fans of the Maquis du Zaire band and finally Maquis Original knew by the name of Mzee Chekecha. His real name was Mwema Mudjanga, he was the band's trumpeter but he had a swagger that eventually gave him the name Mzee Chekecha, he was also one of the directors of Maquis du Zaire and he died on December 6, 2013 in Amana hospital and was buried in Magomeni cemetery Kagera

May they all rest in peace

 

 

Wednesday, December 14, 2022

NI MIAKA 12 TOKA KIFO CHA DR REMMY ONGALA -TUMUOMBEE KWA KUKUMBUKA YALIYOJIRI KATIKA MAZISHI YAKE



Ni miaka 12 toka Dr Remmy alipofariki siku ya Jumapili tarehe 12 Disemba mwaka 2010, kiasi cha saa sita usiku katika hospitali ya  Regency Hospital.  Siku chache kabla ya hapo alikuwa amelazwa Mhimbili akiwa na matatizo ya kisukari na figo, akaonekana amepata nafuu akaruhusiwa kurudi nyumbani, lakini akazidiwa na kupelekwa hospitali ya  Regency, ambako mauti yalimkuta.

Picha za baadhi ya marafiki, na ndugu waliokusanyika nyumbani kwa  Dr Remmy baada ya kusikia msiba  


Cosmas Chidumule  nyuma yake ni Juma Mbizo

Waziri Ally na  Mzee Manyema

Mzee makassy na Mzee Manyema

Mbombo wa Mbomboka

Mohamed Mgoro

Cosmas na Mzee Kungubaya

Mzee Makassy na Waziri Ally

Chiddy Benz na Bombo wa Bomboka

Kally Ongala akiwa na Nyoni, mmiliki wa bendi ya   Super Matimila 

King Kiki akiwa na Shogholo Challi Katibu Mtendaji wa BASATA wakati huo.

Geophrey Kumburu na Farijala Mbutu

Mgosi Mkoloni

 Joseph Mbilinyi aka Sugu

Mohamed Mgoro na Joseph Mbilinyi (Sugu)

Chidumule na Sugu

Hamza Kalala, Mgoro, Chidumule na Sugu

Rashid Pembe, Sugu, Nindi

Tido Mhando , Mgoro

Makassy, Kanku Kelly,  Chidumule



Ratiba ya Mazishi –Alhamisi 16th December 2010

Saa 4 asubuhi –Mwili wa Dr Remmy kutolewa MUhimbili na kuletwa katika viwanja vya Biafra Kinondoni.

 - Maombi

-   Tamasha la muziki (Gospel na rhumba)

-       Kuaga mwili

Saa 8 – Mwili kupelekwa nyumbani kwa marehemu Sinza

Saa 10 – Mazishi katika makaburi ya Sinza

 

Jumatano 15th Disemba 2010  Mkesha wa siku ya mazishi

Seti mbili za vyombo vya muziki vilipangwa nje ya nyumba ya marehemu, na usiku kucha wanamuziki walipiga muziki wakiimba nyimbo nyingi za marehemu na tungo zao nyingine. Kasaloo Kyanga alipanda jukwaani na kuimba nyimbo ambazo walipiga pamoja na marehemu walipokuwa Matimila.


Kadesi mpiga bezi wa zamani wa OSS


Kasaloo Kyanga

Watu wakicheza kumkumbuka marehemu

Mafumu Bilali Bombenga'Super Sax' akipiga Conga




Elly  Chinyama Chiyaza


Mwema Mudjanga, Nkulu Wabangoi, na Kabeya Badu

Makassy Jnr with Mzee Mwema

Mzee Kungubaya



Bushoke Jnr alikuwepo

Mafumu

Malu Stonch

Siku ya mazishi

 Mwili wa Dr Remmy  uliletwa kwenye viwanja vya Biafra kwa gari hili lililosindikizwa na pikipiki mbili za polisi.




Dr Remmy's Coffin



 Mwili ulipofikishwa Biafra, sanduku liliwekwa katika jukwaa maalumu lililokuwa chini ya hema jeupe. Bendi zikaanza kupiga kuomboleza ikiwemo bendi ya Walemavu. Hatimae bendi maalumu ya wanamuziki wa Injili ilipiga wimbo maalumu wa kumlilia Dr Remmy


Watoto na wajukuu wa Dr Remmy







 Kati ya waliohudhuriwa alikuwemo Wazir wa Habari Michezo na Utamaduni Dr Nchimbi, Wabunge wa Kinondoni na Ubungo, Waheshimiwa Iddi Azan na John Mnyika. alikuwepo pia Jaji John Mkwawa, wawakilishi wa BASATA, COSOTA na SHIWATA na wasanii wengi sana,Jambo lililowatoa machozi watu wengi ni pale wimbo alioimba marehemu ulioitwa Siku ya kifo ulipopigwa.







Baada ya hotuba ya Waziri Dr Nchimbi kwa niaba ya serikali na Cosmas Chidumule kwa niaba ya wanamuziki, mamia ya watu walipita mbele ya jeneza kumuaga mpendwa wao.

 Saa nane mwili ukahamia ukumbi wa Kwa Mgiriki, Sinza kwa Remmy ambapo majirani wa marehemu nao walipata nafasi ya kumuaga kabla ya mwili kupelekwa makaburini.

Mazishi







Mke wa Remmy akisindikizwa baada ya mazishi


Kama ilivyopangwa, saa kumi jioni mwili wa DR Remmy ulizikwa Sinza Makaburini. Yakatimia maneno ya wimbo wake wa Siku ya kifo, kuwa <BINADAMU NI NYAMA YA UDONGO>