Ni miaka 12 toka Dr Remmy alipofariki siku ya Jumapili tarehe 12 Disemba mwaka 2010, kiasi cha saa sita usiku katika hospitali ya Regency Hospital. Siku chache kabla ya hapo alikuwa amelazwa Mhimbili akiwa na matatizo ya kisukari na figo, akaonekana amepata nafuu akaruhusiwa kurudi nyumbani, lakini akazidiwa na kupelekwa hospitali ya Regency, ambako mauti yalimkuta.
Picha za baadhi ya marafiki, na ndugu waliokusanyika nyumbani kwa Dr Remmy baada ya kusikia msiba
|
Cosmas Chidumule nyuma yake ni Juma Mbizo |
|
Waziri Ally na Mzee Manyema |
|
Mzee makassy na Mzee Manyema |
|
Mbombo wa Mbomboka |
|
Mohamed Mgoro |
|
Cosmas na Mzee Kungubaya |
|
Mzee Makassy na Waziri Ally |
|
Chiddy Benz na Bombo wa Bomboka |
|
Kally Ongala akiwa na Nyoni, mmiliki wa bendi ya Super Matimila |
|
King Kiki akiwa na Shogholo Challi Katibu Mtendaji wa BASATA wakati huo. |
|
Geophrey Kumburu na Farijala Mbutu |
|
Mgosi Mkoloni |
|
Joseph Mbilinyi aka Sugu |
|
Mohamed Mgoro na Joseph Mbilinyi (Sugu) |
|
Chidumule na Sugu |
|
Hamza Kalala, Mgoro, Chidumule na Sugu |
|
Rashid Pembe, Sugu, Nindi |
|
Tido Mhando , Mgoro |
|
Makassy, Kanku Kelly, Chidumule
|
Ratiba ya Mazishi –Alhamisi 16th
December 2010
Saa 4 asubuhi –Mwili wa Dr Remmy kutolewa MUhimbili na kuletwa katika viwanja vya Biafra Kinondoni.
- Maombi
- Tamasha la muziki (Gospel na rhumba)
- Kuaga mwili
Saa 8 – Mwili kupelekwa nyumbani kwa marehemu Sinza
Saa 10 – Mazishi katika makaburi ya Sinza
Jumatano 15th
Disemba 2010 Mkesha wa siku ya mazishi
Seti mbili za vyombo vya muziki vilipangwa nje ya nyumba ya marehemu, na usiku kucha wanamuziki walipiga muziki wakiimba nyimbo nyingi za marehemu na tungo zao nyingine. Kasaloo Kyanga alipanda jukwaani na kuimba nyimbo ambazo walipiga pamoja na marehemu walipokuwa Matimila.
|
Kadesi mpiga bezi wa zamani wa OSS
|
|
Kasaloo Kyanga |
|
Watu wakicheza kumkumbuka marehemu |
|
Mafumu Bilali Bombenga'Super Sax' akipiga Conga |
|
Elly Chinyama Chiyaza |
|
Mwema Mudjanga, Nkulu Wabangoi, na Kabeya Badu |
|
Makassy Jnr with Mzee Mwema |
|
Mzee Kungubaya |
|
Bushoke Jnr alikuwepo |
|
Mafumu |
|
Malu Stonch |
Siku ya mazishi
Mwili wa Dr Remmy uliletwa kwenye viwanja vya Biafra kwa gari hili lililosindikizwa na pikipiki mbili za polisi.
|
Dr Remmy's Coffin |
Mwili ulipofikishwa Biafra, sanduku liliwekwa katika jukwaa maalumu lililokuwa chini ya hema jeupe. Bendi zikaanza kupiga kuomboleza ikiwemo bendi ya Walemavu. Hatimae bendi maalumu ya wanamuziki wa Injili ilipiga wimbo maalumu wa kumlilia Dr Remmy
|
Watoto na wajukuu wa Dr Remmy |
Kati ya waliohudhuriwa alikuwemo Wazir wa Habari Michezo na Utamaduni Dr Nchimbi, Wabunge wa Kinondoni na Ubungo, Waheshimiwa Iddi Azan na John Mnyika. alikuwepo pia Jaji John Mkwawa, wawakilishi wa BASATA, COSOTA na SHIWATA na wasanii wengi sana,Jambo lililowatoa machozi watu wengi ni pale wimbo alioimba marehemu ulioitwa Siku ya kifo ulipopigwa.
Baada ya hotuba ya Waziri Dr Nchimbi kwa niaba ya serikali na Cosmas Chidumule kwa niaba ya wanamuziki, mamia ya watu walipita mbele ya jeneza kumuaga mpendwa wao.
Saa nane mwili ukahamia ukumbi wa Kwa Mgiriki, Sinza kwa Remmy ambapo majirani wa marehemu nao walipata nafasi ya kumuaga kabla ya mwili kupelekwa makaburini.
Mazishi
|
Mke wa Remmy akisindikizwa baada ya mazishi |
Kama ilivyopangwa, saa kumi jioni mwili wa DR Remmy ulizikwa Sinza Makaburini. Yakatimia maneno ya wimbo wake wa Siku ya kifo, kuwa <BINADAMU NI NYAMA YA UDONGO>
An incredible historical photographs collection. Congratulations !!
ReplyDelete