HAKIKA kumekuwa na utata kuhusu mashindano ninayoyaongelea ni ya mwaka gani. Mashindano ya bendi ambayo yalifahamika kama Top Ten Show yalifanyika mara mbili. Kwa mara ya jkwanza yalifanyika mwaka 1988 na mara ya pili yakafanyika kuanzia tarehe 29 Julai 1989 na kumalizika tarehe 25 Novemba mwaka 1989.
Katika mashindano ya kwanza kila bendi ilipewa uhuuru wa kuchagua nyimbo moja ambayo ishiriki katika mashindano hayo. Katika mashindano ya pili bendi zilipewa nafasi tatu, ya kwanza ni wimbo wowote ambao bendi ingechagua nafasi ya pili ilikuwa ni wimbo wenye'tuni' asili na wimbo wa tatu ulipea jina Afrika Nakulilia.
Mashindano ambayo mnayasikia hapa ni ya shindano la kwanza la 1988. Nategemea wote tunaenda sawa sasa
No comments:
Post a Comment