Monday, June 16, 2014

KIJIWE CHA KITIME SASA PIA KATIKA 93.7 FM REDIONI KILA JUMAPILI

Kila Jumapili kuanzia saa 2 hadi saa 5 usiku kupitia EFM 93.7 Fm, ntakuwa nikikuletelea muziki wa zamani kutoka ulimwenguni kote. Kipindi hiki kitakuwa kikirushwa kupitia radio mpya EFM. Katika kipindi hiki licha ya muziki pia kutakuwa na hadithi mbalimbali kuhusiana na muziki na maisha yalivyokuwa wakati huo. Unaweza kuwasiliana nami kupitia ukurasa wa Facebook huu https://www.facebook.com/pages/ZAMA-Zileeeee/288646357969709 ingia hapa u Like ukurasa huu na kutoa mapendekezo ya unachokitaka. Pia unaweza kuipata redio hii katika mtandao wa internet kupitia http://tunein.com/radio/E-FM-Radio-937-s224740/ haya ingia hapa ufaidi muziki, vichekesho masaa 24.

1 comment:

  1. Tafadhali kaka Kitime niwekee ule wimbo wa kichagga ulioimbwa na mtoto wa injinia wa kiloni aliyeoa mtoto wa kichaga hapo katika payer ya listi ya nyimbo pia ukiniwekea na ule wa National panasonic ulioupiga katika kipindi efm ukasema aliutunga Balisidya utakuwa umenikosha mno ndugu yangu.

    ReplyDelete