Tuesday, October 4, 2011

Eddy Sheggy akikuletea Shakaza 'live'

Jambo ambalo naliona wazi ni kuwa Watanzania wanapenda sana nyimbo za dansi zinazotokana na nyimbo zenye asili ya makabila ya hapa Tanzania. Nikikumbuka nyimbo kama  Mtaulage, Malaine, Nyongise, ambazo ni kazi yangu mwenyewe nikiwa Tancut na Vijana Jazz, kila Munu ave na kwao ya Les Mwenge, Boko wa Kilimanjaro Band, Shakaza ya Bantu  na nyingi nyingine zote zilichukua nafasi ya juu katika anga za muziki wakati wake, na hata sasa. Pengine lingekuwa somo kwa wanamuziki wa Tanzania na kuliangalia hili katika tungo zao. Hebu tumkumbuke Eddy Sheggy hapa akiwa na Bantu, akiimba na ndugu zaki Francis na Christian

9 comments:

  1. Mkuu,

    Habari hii unaijua?


    Nilikuwa napita sternsmusic kuangalia latests releases nikakutana na habari ya kuipua CD ya Vijana Jazz.

    Kwa maelezo zaidi pita:

    http://www.sternsmusic.com/tradewind.php

    Halafu soma hapo chini:

    VIJANA JAZZ BAND


    THE KOKA KOKA SEX BATTALION

    RUMBA, KOKA KOKA & KAMATA SUKUMA: TANZANIA 1975 - 1980

    Release date 14th November, 2011

    The 2nd of January 1975 was a Thursday. Sometime that day, members of the Vijana Jazz Band from Tanzania entered the Hi-Fi Studios at Pioneer House on Government Road in Nairobi, Kenya, and recorded 6 tracks under the pseudonym of the Koka Koka Sex Battalion. Along with Rumba, Kamata Sukuma (grab 'n' push), Koka Koka was a style of music, but the band's name was a scam.

    Vijana translates as 'youth' and refers to the group's sponsorship by Umoja wa Vijana, the youth wing of Tanzania's ruling political party. Recently galvanized by the addition of singer/composer Hemedi Maneti, Vijana Jazz were a successful group with many singles already available and the label, conscious of this, was keen not to flood the market. The band on the other hand, with a trip from Tanzania that took at least a day and a night, were keen to get paid as much as they could, and in Kenya they only got paid for what they recorded. Thus they presented the 6 tracks as if by a new, hot and previously unrecorded band and the label, taking their eye off the ball, handed over the cash.

    It wasn't a particularly impenetrable scam, Koka Koka was known as the signature style of Vijana Jazz and both “Koka Koka!” and “Sex Battalion!” were common shout-outs within their recordings. In addition the writers credited on the session were known members of the group. But whatever exactly happened that day, 35 years later we are the lucky beneficiaries as two of those cuts are grouped with other hits and rarities of Vijana Jazz to give a fascinating glimpse of the unique energy that was East African music in the mid 1970s as performed by one of the best bands of the time.

    Mdau Sokomoko Damu, Helsinki, Finland.

    ReplyDelete
  2. Habari hii ninataarifa nayo mkuu, Sterns waliniandikia ilikuhakiki baadhi ya majina na kuulizia kama nina picha za wanamuziki hawa. Kuna bendi nyingi za Tanzania zilienda Kenya na kufanya recording kisha kulipwa na hivyo kuwa wameuza kazi zao na hasa kundi kama hili au kama ilivyokuwa Black Warriors waliokuwa 'wametoroka' toka Sikinde.

    ReplyDelete
  3. Mkuu,

    Asante kwa majibu.

    Hili suala la bendi zetu kwenda Nairobi kurekodi linaweza kuwa mada nzuri sana ya majadiliano. Kuna maswali kdahaa yanayojitokeza katika hili:

    1: Kwa nini Tanzania haikuwa na studio ya kufyatulia santuri?

    2: Ile studio ya kufyatulia santuri ya TFC pale Kinjitonyama kwa nini haikufanya kazi hadi leo?

    3: Kwa nini "watoro" wa kwenda kurekodi Nairobi walikuwa ni bendi za serikali? Marehemu Mbaraka Mwishehe na Super Volcano na Mzee Makassi walirekodi Nairobi lakini "hawakutoroka". Swali la nne linakuja:

    4: Kwani serikali ilikuwa hairuhusu wanamuziki kwenda kurekodi Nairobi hadi "watoroke"?

    5: Kwa nini studio za kurekodi kama EMI, Polydol, ASL na mengineyo yalikuwa na studio Nairobi lakini hawakuwa na studio Tanzania ambapo kulikuwa na bendi nyingi na soko kubwa la muziki?

    6: Je wanamuziki wana haki ya kwenda kudai au kuomba miziki waliyorekodiwa RTD na kuifyatua upya kama santuri au CD?

    Haya ni baadhi tu ya maswali yaliyonijia haraka haraka kichwani. Natumaini wewe pamoja na wengine wengi mtakuwa na majibu na maswali zaidi katika mada hii.

    Asante,

    Mdau, Sokomoko Damu, Helsinki, Finland.

    ReplyDelete
  4. R.I.P,Eddy Sheggy. Sauti yake itaendelea kuishi.

    ReplyDelete
  5. 1/2.. Tanzania ilikuwa na mpango wa kutengeneza kiwandacha kuchapa sahani za santuri chini ya TFC. Kilikuwa kiwe katika eneo ambalo kiko Chuo Kikuu cha Uandishi. Mkopo ulitoka TIB, kizungumkuti kilichotokea ni hadithi ndefu lakini studio hiyo haikukamilika na hatimae majengo yamegeuzwa madarasa ya Chuo Kikuu.
    3.Mpaka wa Tanzania na Kenya ulikuwa umefungwa hivyo wote waliokwenda huko wakati huo walikuwa 'watoro' hata Mbaraka pia.
    5. Kumbuka kuwa siasa za Tanzania wakati huo hazikuruhusu uwekezaji binafsi katika sekta hiyo ya muziki, mambo ya muziki yalikuwa chini ya TFC Tanzania Film Company.
    6. Wengi huchukua nyimbo zao na kuziuza au kufyatua CD wanapoamua

    ReplyDelete
  6. Mkuu,

    Asante kwa majibu.

    TFC pia walikuwa na eneo pale Kijitonyama nyuma ya Kijiji cha Makumbusho ambalo lilikuwa liwe studio ya kufyatulia santuri. Lakini kwa sababu ambazo haiko wazi mpaka leo studio haijajengwa na sijui lile eneo wanalitumia kufanyia nini?

    TFC walikuwa na studio kule Msasani ambako siku hizi imekuwa Cine Club. Marehemu Kakele aliwahi kurekodiwa kwenye zile Studio mwanzoni mwa miaka ya 80. Kilimanjaro Band kwenye lile album la chakacha ya Liwache Shamba Limeshakushinda Watalilima Wenziyo walirekodiwa katika ile studio ya Msasani, naomba umuulize Mabruki kwa usahihi zaidi wa taarifa hii. Marehemu Issa Matona zile album zake Leo ni leo na Uliye Naye Umzuie ilirekodiwa kwenye zile studio za Msasani. Sijui wingi wa santuri zilizorekodiwa kwenye ile studio. Naomba ukikutana na Mzee Ndumbalo umuulizie juu ya hili.

    Mpaka na Kenya tulikuwa tumeufunga kuanzia 1977 baada ya kuvunjika kwa Shirikisho la Nchi za Afrika Mashariki. Hivyo Vijana Jazz "Sex Battalion" hawakutoroka wakati mpaka umefungwa. Tunaweza kuwaita "watoro" kwa sababu waliondoka bila kumtaarifu mwajiri wao na wakarekodi bila ridhaa ya wenzao kadhalika ya mwajiri wao.

    Mkuu, mawazo na maamuzi yakiwa ya njia moja kama yalivyokuwa wakati wa ule yanaweza kuwa na madhara sana mathalani hili la kutokuwa na studio za kufyatulia santuri. Hapa kuna dhana ya kudharau kazi za wengine na kuziona siyo kazi hivyo kuzidhibiti mapana yake. Unaweza kusikia kiongozi au maamuma yoyote anasema huku mapovu ya hasira yanamtoka "..Yaani tuinvest mamilioni ya pesa kwenye studio ya muziki badala ya kujenga madarasa? Upumbavu gani huu!?..Let's look at our priorities, eti wennzangu do we really need a music studio!? Eeh jamani eti muziki uchukue mamilioni ya kodi ya walala hoi!?.." Akimaliza anapozi kuwaangalia anaoongea nao huku anatoa tabasamu la kebehi. Wasikilizaji wanaafikiana naye wanaona mantiki ya pingamizi yake. Mkuu, nakuhakikishia huo ndiyo mwisho wa fikra za walio wengi wa wakati ule kuhusu muziki na ndiyo sababu hakukuwa na studio za kufyatulia santuli. Lakini kulikuwa na kiwanda cha kutengeneza Dudu roof National 277, Matshushita Electric Company, Pugu Road, Dar es Salaam na Philips, Arusha kwa hiyo mkitaka muziki mtaupata toka RTD kupitia kwenye Dudu Proof 277 au Philips ndiyo yenyewe, sauti safi, sauti kubwa!

    Sasa zimekuja studio nyingi kama utitiri. Zaidi ya muziki wa Injili nasema wazi katika zama hii ya utitiri wa studio sijasikia muziki wowote wa maana uliorekodiwa zaidi ya ule wa zamani.

    Mdau, Sokomoko Damu, Helsinki, Finland.

    ReplyDelete
  7. Hilo eneo la Kijitonyama ndipo sasa Chuo Kikuu cha Uandishi wa Habari

    ReplyDelete
  8. Mkuu,

    Asante kwa kubadilishana mawazo.

    Nakutakia weekend njema,

    Mdau, Sokomoko Damu, Helsinki, Finland.

    ReplyDelete
  9. Hivi jamani ni kwamba hamjaifungua iyo link ya wimbo wa Vijana jazz au vipi? Jerry Nashon is a legend jamani. Mambo aliyofanya katika umri wa ujana ni mazito mno katika ulimwengu wa mziki. Message ilitosha kabisa. Halafu mbona mziki na picha zipo clear sana ingawa imerekodiwa live? Ivi hii technology ilishakuwepo wakati huo. Priceless stuff

    ReplyDelete