Saturday, May 31, 2014

ALHAMISI MAY 31, 1990. SIKU ALIPOFARIKI HEMED MANETI ULAYA

Tarehe 31 May 1990 siku ya Alhamisi majira ya saa kumi na moja jioni, ndipo alipofariki Hemed Maneti katika hospitali ya Mwananyamala. Hemed wakati huo alikuwa ni mwanamuziki muimbaji na Kiongozi wa Vijana Jazz Band. Alikuwa ameanza kuwa na matatizo ya afya miezi kadhaa kabla ya hapo na  hatimae kupelekwa Tanga kwa ajili ya matibabu. Hali yake ilipozidi kuwa mbaya alirudishwa kwa ndege  kuwasili Dar Jumatano 30 May na kupelekwa moja kwa moja hospitali ya Mwananyamala ambapo alilala na kufariki kesho yake. Marehemu alisafirishwa kwenda kuzikwa Tanga siku moja baadae.
Wimbo wa mwisho kurekodi ulikuwa wimbo wa kufunguliwa kwa Mandela uliotungwa na John Kitime
Hawa walikuwepo mortuary siku ya kuondoka na mwili wa marehemu kwa ajili ya kupeleka Tanga, wa mwisho kulia Mzee Jacob John, mwenye jacket jekundu marehemu Mzee Faya

No comments:

Post a Comment