Thursday, April 4, 2013

UNAUKUMBUKA WIMBO BB69? SIKILIZA HAPA


Ngaiyaoo Ngaiyaoo
Unipe mama, roho yangu
Nifurahi nayo, mpenzi wangu
Lakini sipendi kuchelewa bure
Wimbo huu nilipousikia mara ya kwanza kupitia santuri ulinigusa mahala ambapo mpaka leo umeacha nafasi fulani. Wimbo huu ulitungwa na Jeannot Bombenga na ukapigwa na na African Jazz group, African Jazz wakati huu ilikuwa imekimbiwa na yule mwamba wa muziki Afrika Grand Kalle ambae aliondoka na kundi Volcan Ni Beto Ba kwenda Ufaransa. Ilikuwa ni kama alama kuwa African Jazz ilikuwa inaweza kuendelea hata bila Mzee Kalle, huyu asije changanywa na Pepe Kaleni watu wawili tofauti sana.

1 comment:

  1. All the time favorite, all he time classic!! Respect JFK

    ReplyDelete