Wednesday, April 3, 2013

BOLINGO YA TELEPHONE(1967)....WIMBO MTAAMU...maana yake inaendelea kudumu



Wimbo huu nilipousikia mara ya kwanza miaka ya 68/69 niliupenda na mpaka leo bado naupenda sana. Wimbo huu ulitungwa na mwanamuziki Zizi wa bendi ya Los Nickelos, sijui kwa ajili ya ugumu wa jina au kwa kuwa sikumbuki wimbo mwingine uliotolewa na bendi hii na kuchanganya sana vijana wa wakati ule, lakini hii bendi haikuwa maarufu sana na wala sijasikia ikitajwa na watu wengi mpaka leo japo huo wimbo ulihamasisha bendi kadhaa ikiwemo Morogoro Jazz Band kutunga wimbo wa visa vya mapenzi katika simu. Na vituko vya mapenzi kwenye simu bado vinaendelea kama ilivyoimbwa miaka 40 iliyopita .HUO NDIO UTUNZI ULIOTUKUKA

No comments:

Post a Comment