Mzee Abdallah Hatibu (katikati) |
Nyota Ndogo ni jina maarufu sana Afrika Mashariki, ni mwanadada
mwanamuziki wnenye sauti tamu sana, kati ya vibao vyake vyote nikiri kuwa wimbo
wake wa Watu na Viatu ambao ulishinda tuzo katika Tanzania Music Awards 2007 ni wimbo ninaoupenda sana,
pia huyu binti ambaye amekwisha toa album kadhaa zikiwemo Chereko, Nimetoka
Mbali na Mpenzi alizaliwa 1981 na akapewa jina la Mwanaisha Abdallah.
Mwanaisha alizaliwa Mombasa hakumaliza shule na katika kazi alizopitia ni msaidizi wa
nyumbani. Katika kuonyesha tena kuwa wanamuziki wengine, muziki umo kwenye damu,
baba wa binti huyu alikuwa mwanamuziki. Katika maelezo ya rasmi ya Nyota Ndogo
baba yake alikuwa mwanamuziki wa bendi moja wapo Mombasa na aliitwa Abdallaha
Hatibu. Blog ya www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.com
ambayo ni maarufu kwa kutafiti historia ya wanamuziki wa zamani wa hapa nchini
iliweka historia fupi ya kundi maarufu la Jamhuri Jazz Band, pamoja na picha ya
mmoja wa wanamuziki wa bendi hiyo aliyeitwa Abdallah Hatibu. Mwanamuziki mahiri
Profesa Abbu Omari aliyeko Japan ambaye pamoja na bendi nyingi alizopigia pia
alipiga Les Wanyika, na Simba wa Nyika alikuwa na maelezo ya ziada kuhusu Mzee
Abdallah Hatibu. Haya ndiyo aliyoyasema……Mkuu Kitime katika picha za hawa wakongwe wa Jamhuri jazz hapo kati kati
kuna mwanamuziki alikuwa anaitwa Abdallah Hatibu, sisi tulikuwa tunamjua kama
mzee Abdallah,alikwisha fariki miaka kama mitatu iliyopita,Huyu ni baba wa
waanamuziki wawili mashuhuri wa Mombasa mmoja msichana Nyota ndogo na mvulana
Juma Tutu, Mzee Abdallah alizikwa kwao Muheza baada ya kuishi Mombasa na
Nairobi kwa miaka mingi,hata mimi niliwahi kuishi nae jengo moja Nairobi 1982, Mzee
huyu alikuwa mkali kwa gitaa nadhani hata kushinda Michael Vicent, nadhani
huenda ikawa yeye ndiye aliyemfundisha Michael kupiga gita, niliwahi kumuuliza
kuhusu huyu Michael na akasema huyo alikuwa mtoto mdogo tu ki miziki kwake. Kwa
kweli huyu mzee Abdallah alikuwa mkali sana kwa gitaa Mombasa nzima na Nairobi
alijulikana. …..Abbu Omar Tokyo,Japan
Juma Tutu |
Nyota Ndogo |
Pia kadri ya website ya Juma Tutu , (JUMA TUTU) familia yao walizaliwa sita
sehemu ya Majengo huko Mombasa, baba yake alikuwa mpiga gitaa la solo katika
bendi ya Simba wa Nyika katika Club ya Sabasaba pale Mombasa, mama yao
Christine Mungala pia alikuwa muimbaji katika kwaya ya kanisani. Dada zake wawili Nyota Ndogo na Leila pia ni wanamuziki mahiri.
No comments:
Post a Comment