Harrison Siwale (Jamhuri Jazz Band), Mbaraka Mwinyshehe(Morogoro Jazz band), Abdul Mketema(Morogoro Jazz Band) |
WANAMUZIKI wetu wakali wakiwa katika picha pamoja. Picha hii ina maana nyingi sana moja likiwa ni umoja uliokuwa unawezekana kwa wanamuziki wa bendi mbalimbali. Mbaraka Mwinyshehe alikuwa mpiga solo na muimbaji wa Morogoro Jazz band wakati huu, Abdul Mketema alikuwa mpiga saxophone na mtunzi wa nyimbo kadhaa za Morogoro Jazz band, Harrison Siwale alikuwa mpiga rythm ambaye aliwika sana alipokuwa Jamhuri Jazz Band ya Tanga. Si hivyo tu Siwale na Mbaraka wote katika wakati tofauti walipitia Atomic Jazz ya Tanga, kuna wimbo ambao uliwahi kurekodiwa na Mbaraka wakati akiwa Atomic Jazz baada ya kuhama Morogoro Jazz kwa muda. Zamani bendi zilikuwa na udugu, Dar Jazz walikuwa kila wakienda Morogoro wanakuwa wageni wa Cuban Marimba, Fauvette walipoingia Dar es Salaam walipokelewa na Western Jazz.
No comments:
Post a Comment