Hatua chache baada ukiingia katika lango la makaburi ya
Kinondoni, kushoto kwako utalikuta kaburi la msanii Steven Kanumba. Kanumba
akiwa na umri mdogo wa miaka 28, alifariki ghafla katika mazingira ambayo yamepelekea msanii mwenzie Elizabeth Michael kuwa katika kesi ya
kutuhumiwa mauaji ya msanii huyu aliyekuwa mahiri katika kazi yake ya usanii wa
kuigiza na pia aliyekuwa na sura ya kupendeza yenye mvuto, wengi tunamfahamu kwani bado
yuko katika mawazo yetu kutokana na kazi zake kuwa bado zikiendelea kuonekana
katika vyombo mbalimbali vya utangazaji. Jirani kabisa ya kaburi la Kanumba,
kuna kaburi moja la zamani sana la mwanamuziki Isihaka Gobyy. huyu alikuwa mwanamuziki wa Orchestra
Makassy katika miaka ya 1976/77. Gobby nae alikuwa na sifa zilizofanana sana na
zile za Kanumba. Kwanza alikuwa mwanamuziki muimbaji mahiri sana, pili alikuwa
na sura yenye kuvutia sana.
Wakati huo
bendi ya Makassy ikiwa na makao makuu ukumbi wa Hunters, ikiwa na ushindani
mkubwa kutoka kwa bendi ya Bana Ngenge iliyokuwa katika ukumbi mwingine jirani wa Savannah, na Orchestra Maquis du Zaire iliyokuwa ikipiga katika ukumbi wa Resort Kimara.
Gobby nae alikufa kifo cha ghafla akiwa na miaka 28, kwa kuuwawa kwa kupigwa na
hatimae kuchinjwa kama kuku katika ugomvi uliovuma wakati huo kuwa ulikuwa
ukihusu mapenzi. Hakuna taarifa za kuwahi kukamatwa aliyemfanyia Gobby unyama
huu uliopoteza maisha yake mwanamuziki huyu kijana.
Mungu awalaze Kanumba na Gobby Pema Peponi
ama kweli hayo ni maajabu....
ReplyDelete