Tuesday, December 6, 2011

Kumbukumbu ya Brig Gen Moses Nnauye

Leo ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mzee Nnauye (5/7/1937-6/12/2001). Mzee Nnauye alikuwa mwanamuziki mzuri sana na alitumia sana muziki katika harakati za kupigania uhuru. Alianzisha na kuendeleza vikundi vingi vya kwaya, taarab na bendi na wasanii wengi sana waligunduliwa nae na kulelewa kama wanawe kutokana na kutaka waendelee katika muziki. 
Mzee Nnauye wakati akiwa Mkuu wa Mkoa Singida
Kila nikisikia wimbo wa Guantanamela huwa namkumbuka Mzee huyu ambaye kwa mara ya kwanza nilikuwa karibu nae mwaka 1987, wakati niko katika bendi ya Tancut Almasi, wakati huo tukiwa tumepiga kambi ya miezi kadhaa Dodoma Hotel. Alitukaribisha wanamuziki kadhaa nyumbani kwake na kutuonyesha santuri(LP) ya wimbo original version ya Guantanamela. Kisha akamuita mwanae atupigie wimbo huo katika kinanda kuanzia hapo kila mara nilikuwa karibu na mzee huyu. Mzee Nnauye ndiye aliyegundua kipaji cha Mheshimiwa Capt John Komba na kumtoa katika kazi yake ya ualimu na kumuingiza jeshini kuendeleza kipaji chake cha uimbaji, matokeo yake wote tunayajua. Wakati akiwa Singida aliweza kuwavuta wanamuziki kadhaa kutoka Black Star na Lucky Star za Tanga, na wanamuziki kadhaa akiwemo Wazir Ally wa Kilimanjaro Band walihamia huko na kuwa wanamuziki wa bendi King'ita Ngoma iliyokuweko Singida wakati huo. Wote tunajua umahiri wa Waziri Ally.
Katika mazungumzo yetu ya mara ya mwisho alikuwa anatamani sana kulileta lile kundi la Africando, mapigo ya Kilatino ya kundi hili yalimfurahisha sana na alikuwa anaona itakuwa bora kwa Watanzania kupata vionjo tofauti na vilivyozoeleka ambavyo vilikuwa ni kutoka kwa wanamuziki wa Soukus tu kutoka Jamhuri ya Congo.
Mungu amlaze pema Mzee Moses Nnauye
Amen

9 comments:

  1. Ingawa bado nilikuwa ,mdogo std 6&7 1970-71 nilikua nikisomea Nyerere Rd pri-sch namkumbuka sana mzee huyu,hasa kwakua alikua boss wa mzee wangu R.M Mwinjuma akiwa ofisa mkuu wa ujamaa na ushirika mkoa,wote walipenda muziki sana.katika nyumba alioishi singida niliingia nyumba hio hata kabla mzee Mnauye kuja alikua mkuu wa mkoa mzee Kapilima nae pia mpenzi mkubwa wa muziki kulikua na piano kubwa pale ukumbini nikipenda sana kucheza nayo na ndio chanzo cha muziki wangu kuimba na kupiga gitaa(mazingazinga)

    ReplyDelete
  2. mfano mzuri wa kutumia kipaji na nafasi yke kunufaisha Watanzania wenzake. Sikupata kuwa karibunaye lakini nakumbuka nili-produce wimbo wa Spare Tyre wa John Mjema. Mzee alipousikia alimwita na kuahidi kumsaidia, baadae alimtafutia kazi serikalini. tatzio lilikuwa kwa John Mjema kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.

    ReplyDelete
  3. RIP Comrade Moses Nnauye. Nilipokuwa nikifanya kazi Wizara ya Utamaduni 1986, nilikuwa mmoja wa watu sita tuliokwenda Dodoma kenye mashindano ya ngoma za kiasili/kijadi za Tanzania. Wakati huo Comrade Moses hakuweko Dodoma (alikuwa amesafiri). Hata hivyo aliwacha ujumbe kwa mkwewe kuwa Mrs Nnauye aje kutuchukua hoteli ili twende kwake kwa dinner. Baada ya mlo mzuri na soda na maji ya matunda, Mrs Nnauye alituomba radhi kwa niaba ya Moses Nnauye kwa kuwa Comrade Nnauye hakuweza kuwa na sisi kwa sababu ambazo hazikuweza kuzuilika (za kikazi). Brigadier Nnauye alikuwa ni mnadharia (theoritician) na mchambuzi (analyst) mzuri sana wa masuala ya siasa. Muhimu zaidi, alikuwa committed 100% kwa maendeleo ya Watanzania. Nilikutana naye kwa mara ya mwisho mwaka 2000 Arusha (Impala Hotel) alipokuwa safarini mikoani ili kuimarisha matawi ya CCM. Alikuwa anaonekana kuwa anaumwa au amechoka, lakini kwa watu commited kama yeye ugonja si sababu ya kupumzika (inanikumbusha Mwalimu Nyerere mwaka 1999 alipokuwa katika mazungumzo ya amani ya Burundi, Arusha aliposhinikizwa na madaktari wake akubali kwenda UK kwa matibabu na Comrade AbdulRahman M Babu ambaye alikuwa anaandika kuhusu masuala ya kisiasa na kijamii na biografia yake mpaka ikabidi naye ashinikizwe kwenda hospitali na kutangulia mbele ya haki).Tunamwomba Mwenyezi Mungu amweke mahali pema peponi. Amin.

    ReplyDelete
  4. A revolutionary thinker and a true patriot. Ewe Mola Muumba wetu, tunakuomba uilaze roho ya M Nnauye mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  5. Namkumbuka alikua ni kiongozi mwadilifu,mpenda kazi na aliejituma.Ni mpenda muziki na akipiga mariba.Alijito kwa chama chake nawananchi wake.Mola ailaze pema roho yake.Amiin.

    ReplyDelete
  6. MZEE NNAUYE SIMFAHAMU ILA KWA JINSI NILIVYOSIKILIZA SIMULIZI NITAPENDA KUMFAHAMU ZAIDI UNDANI, KWA KUWA SIMULIZI YA MZEE MAKAMBA IMENIVUTIA NA KUNITOA MACHOZI.

    ReplyDelete
  7. MZEE NNAUYE SIMFAHAMU lakini nimesikiliza SIMULIZI kutoka mzee MAKAMBA na kushawishika KUMFAHAMU ZAIDI mzee huyu ambaye Ni mwanasiasa mkongwe nchini.

    ReplyDelete
  8. very interesting ..R.I.P Mr Moses Nnyauye

    ReplyDelete