Tuesday, March 29, 2011

The Sparks

Toka kushoto Omary Mgogo, Mohamed Ibuni, Lameck
Hili lilikuwa kundi lililokuwa likipiga pale Gateways (Mnazi Mmoja). Kundi zima lilikuwa la wanamuziki wafuatao, kwenye  solo gitaa alikuwa  Mike Muhuto, rythm gitaa alikuweko Lamek na Jacob Ubwe, besi liliungurumishwa na Remmy(huyu alikuja hata kupigia Varda Arts lile kundi machachari la vijana wa Kihindi), drums George Muhuto, sax Mohamed Ibuni, wakati squad ya waimbaji ilikuwa Omari Mgogo, Stella Amry, Steven Jojo na Huluka Said(wakati huo akijulikana kama Little James Brown), kundi hili baadae likaja kuwa The Comets.

3 comments:

  1. Thanks again John.

    I remember the song "Tunakuomba Rabi Mola Yea Yea Yeah, Sparks Oyee, Yea Yea Yeah Eh "

    Hao walikuwa ndugu zangu, watoto wa Magomeni na wa Mission Quarters ( Misheni Kota)

    ReplyDelete
  2. Ahsante sana kwa kunikumbusha ujana wangu. Nilikuwa week end lazima niwe gateways au splendid ilipokuwa inapiga the rifters. Habati nzuri ninazo nyimbo zote za rifters, sparks, comets na sunbuurst ( hawa walikuwa wakipiga kuanzia saa tisa bahari beach na kabla yao wanapiga the comets. By the way Huluka tulikuwa tunamwita Huck Brown. Vipi jamaa kam kina Omar Din ( alikuwa na Super Bantou pale new palace- bado anaishi?
    Hamissi Delgado

    ReplyDelete
  3. Bwana Delgado naomba tuwasiliane kupitia jkitime@gmail.com

    ReplyDelete