Thursday, October 6, 2011

Tancut Almasi Orchestra na Kashasha

Kuanzia album ya kwanza ya Tancut Almasi Orchestra , bendi iliendelea kutoa vibao vilivyoweza kudumu katika kumbukumbu za wote waliovizisikia kuanzia enzi hizo, album ya kwanza ilikuwa na nyimbo kama vile, Nimemkaribisha nyoka(Kasaloo Kyanga), Kashasha(Kyanga Songa), Tutasele (Kasaloo), Mtaulage(John Kitime), Big Four(Utunzi wa wimbo huu ulileta utata kwani ulianza kwa ugomvi kwa Mamado Kanjanika kudai kuwa aliutunga yeye wakati akina Kasaloo na Kyanga wakidai wameutunga wao. Lakini hatimae akina Kasaloo waliacha ugomvi huo na Mamado hutajwa kama mtunzi wa wimbo huu. Hebu angalia mambo yalivyokuwa wakati Kashasha likipigwa. Niko hapo na miwani kubwa nikiungurumisha rhythm guitar

9 comments:

  1. ASANTE SANA UNCLE KITIME,NAONA RAHA SANA HAPA US,YANI NIKITOKA ZANGU KUBEBA BOX MIMI MOJA KWA MOJA NYUMBANI NIKIFIKA NAOGA, NATIZAMA KIDOGO HLN TV LIVE COVERAGE YA MICHAEL JACKSON TRIAL HUKU NAPATA MSOSI,NIKIMALIZA MOJA KWA MOJA HAPA KWAKO NAKULA DANSI MPAKA UCKU WA MANANE....NAIPENDA SANA TUNCUT JAPO NILIOONA MARA CHACHE NIKISOMA MBEYA IKIJA KUPIGA COMMUNITY CENTRE NA SOKOINE STADIUM,SASA NAHITAJI SANA ALBUM ZA TUNCUT HASA HIYO YA WIMBO KUMBE NIMEMKARBISHA NYOKA,NILIKUJA DAR LAKINI KWENYE MADUKA YA MUZIKI HUPATI NYIMBO ZA TANCUT,NILIELEKEZWA NA ZOMBOKO NIKUTAFUTE WEWE AU ABDUL SALVADOR FATHER KIDEVU,UTANISAIDIAJE,E MAIL ADDRESS YANGU NI diadolla@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  2. Naomba msaada kwenye tuta kaka,-Nani alipiga Bass katika mwimbo huo,-na kama yupo hai anapigia band gani kwa wakti huu?

    ReplyDelete
  3. Bass katika wimbo huu lilipigwa na Amani Ngenzi, ambae pamoja na kuwa hakuwahi kupigia bendi yoyote nje ya Iringa alikuja kuwa mpigaji bora sana. Amani Ngenzi alifariki miaka ya 90.

    ReplyDelete
  4. KASALOO NA KYANGA KIUKWELI WALIKUA WANALICHANGAMSHA SANA JUKWAA LA TANCUT ALMAS WANA FIMBO LUGODA NA MANGARA DANCE

    R.I.P.BOTH OF THEM,NAOMBA TUWEKEE KIBAO KUMBE NIMEMKARIBISHA NYOKA NAJUA HUTAKIKOSA,JAPO TUKISIKILIZE KWENYE PLAY LIST KAMA HUNA KIDEO CHAKE

    ReplyDelete
  5. Asante Sana uncle Kitime. Tulikutwa kama miezi matatu hapa Carabash, Mwenge. Kwa sasa ni Italy kwa muda. Naomba kuuliza, KAWELEE yuko wapi siku hizi? Bado anapiga Muziki.

    Blog yako inatukumbusha mbali. Ikiwezekana uwe unaweka matangozo kunyesha bendi zinazopiga musiki wa zamani zinapiga wapi week-ends.

    ReplyDelete
  6. Kawelee Mutimwana yuko London Uingereza na bado anapiga muziki katika bendi yake ya Africa Jambo Band

    ReplyDelete
  7. Vijana hawa wa Tancut nilikuwa nawakubali ile mbaya.

    ReplyDelete
  8. Asante sana Kitine kwa blog yako hii,mimi naulizia hivi Harila Tongolanga na bendi yake ya Makondeko Musica, yuko wapi? naweza ukanipatia contacts zake?

    ReplyDelete