Friday, September 9, 2011

Seleman Kasaloo Kyanga


Mwanamuziki Selemani Kasaloo Kyanga ambaye alikuwa pacha wa Kyanga Songa walizaliwa Kongo mwaka 1957. Walikuwa ni nyota katika bendi zote walizopitia nchini zikiwamo, Matimila, Makassy, Maquis, Sambulumaa, Ngorongoro Heroes, Tancut Alimas, Sandton Sound, Kalunde Band  na bendi nyingine nyingi . Kasaloo aliyetangulia kuingia nchini akifuatana na Skassy Kasambula mwaka wa 1980, aliweza kutingisha anga za muziki kuanzia pale aliposikika kwenye nyimbo zilizorekodiwa na Super Matimila. Kyanga nae akisindikizana na Issa Nundu walifuatia na sauti zao kuanza kusikika katika recording ya Orchestra Makassy na zile nyimbo Olenge,Bembeya,na pia kuimba na Masiya Radi katika nyimbo Tunagombana Bure. Kyanga alifia Kenya na Kasaloo amefariki jijini Dar es Salaam kutokana na mapafu yake kujaa maji. Alikuwa Sandton Sound Band aliyojiunga nayo akitokea Kalunde Band. Kamati ya msiba wa Kasaloo ikiongozwa na King Kiki yenye wajumbe Mzee Mapili, Mzee Manyema, Mbombo wa Mbomboka, Deo Mwanambilimbi, Mzee Jerome, Matunda, Mzee Peter George na John Kitime, imetoa ratiba ifuatayo.

Saa 3-5...Kutayarisha mwili katika hospitali ya Mwananyamala
Saa 7-9 Kuagwa na dua nyumbani kwa marehemu Tiptop Manzese
Saa 10 Mazishi Sinza Makaburini.
Marehemu ameacha wake wawili na watoto 6.



Seleman Kasaloo alibadili dini na kuwa Muislamu katika miaka yake ya mwisho ya maisha, na kutoa wosia kuwa azikwe kwa taratibu za dini yake ya Kiislam.

5 comments:

  1. Kwa heri Kasaloo! Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen

    ReplyDelete
  2. Mungu akupokee na kukuweka pema mjomba Kasaloo. Nilikuwa mpenzi wako mkubwa wa tungo zako kama Karubandika, Nimemkaribisha nyoka, na Masafa Marefu.

    Mungu awe nawe daima!

    ReplyDelete
  3. Kasaloo Kyanga atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika muziki wa dansi Tanzania,Mimi binafsi nilikuwa mpenzi sana wa uimbaji wake na pia mpenzi mkubwa wa muziki wa Tancut Almasi Orch.Kweli dunia siyo yetu sisi sote tunapita tu.
    R.I.P Kasaloo Kyanga.
    Abbu Omar Prof.Jnr(Mwanamuziki)Tokyo,Japan.

    ReplyDelete
  4. mungu akuweke mahali pema peponi Kasalo, nakukumbuka sana hasa ulipokua na Tancut, lakini kumbukumbu ya karibu ni ile siku ulipokua na kalunde pale Cine Club, tulikaa meza moja na kukumbushana mengi ya Tancut Almas, na nakumbuka tuliimba wimbo wa masafa marefu miminikiwa na hawa kasomo kwenye mic.

    ReplyDelete
  5. RIP Kasaloo...sikujua jamaani! RIP legend!!!

    ReplyDelete