Friday, September 30, 2011

Jerry Nashon


9 comments:

  1. Bwana kitime naomba sana hii historia ya muziki wa dansi isipotehe ningependa kuwasiliana nawe baada ya wiki tatu asante sana yaani umetukumbusha mbali sana,
    yosef

    ReplyDelete
  2. KAKA J KITIME NAKUPA HONGERA SANA KUJARIBU KUWAKUMBUKA WALIOPITA KTK AWAMU TOFAUTI ZA MZIKI WA KWETU INGAWA WALIO WENGI WANAWASAHAU.

    ReplyDelete
  3. aaah kaka kitime leo umeniamkia mimi nini?yani umeweka vitu vya watu wangu wote,masikini marehemu jerry nashon dudumizi mungu amuweke mahali panapofaa huko aliko,huyu mtu alikuwa na kipaji sana cha kutunga nyimbo,nikimsikiliza badi bakule wa tot band sijui kama bado ipo huwa namkumbuka sana marehemu jerry,sauti ya bakule ndio kama ya jerry vilele,ni kama msanii wa bongo fleva marlow alivyo na sauti ya fresh jumbe mzee wa japan,leo ukimchukua marlaw ukamuweka pale msondo au sikinde then ukamwambie aimbe nyimbo alizoimba fresh utakubaliana na mimi.Pia kwenye video hapo namuona kipenzi changu mwingine Shaban Yohana wanted kwenye mpini wa solo,sijui nae yuko wapi maskini.

    SAYZ MDAU USA,TUNAOMBA TV IWE HEWANI MASAA 24 KWENYE INTERNET

    ReplyDelete
  4. ASANTE NIMEIONA LIST YA NYIMBO ZIKIWEMO ZA TANCUT HAPO PEMBENI KULIA,YANI LEO NI BANDIKA BANDUA TU HAPA NABURUDIKA KWA HIYO PLAY LIST KALI

    THANKS.SAYZ MDAU WA US

    ReplyDelete
  5. Mze wa Ndekule siyo kama hawa wanamuziki tunawasahau isipokuwa kuna vita baridi kati ya presenters na ma dj wa huko Bongo wanafanya chini juu ili huu muziki wetu wa asili usaulike na kukuza fleva. Si unaona mwenyewe ukisikilize hizi za zamani jinsi unavyosisimuka kuliko fleva za zamani. Tatizo Bongo hawajui tu kuwa kitu original ni original hata upige vita stori inabaki pale pale tu. Huwezi kuua muziki wetu wa asili na kukuza fleva ni kitu ambacho hata sie wengi tulio huko we don't even like fleva tunasikiliza tu basi.

    ReplyDelete
  6. Bw. Kitime najuwa ulikuwa Tancut lakini nakukumbuka wakati wa Sagha Rhumba pale Vijana Social. Mze mzima ulikuwa na mbwembwe za ajabu, kwa kucheza na gitaa la rythim mze wangu unatisha. Hongera!

    Katika huu wimbo wa "Mtatumaliza,"Jerry aliimba.

    "....Basi kazi kwetu sisi kina kakaaa
    Basi kazi kwetu kina ...... sisi(naomba unijazie) tukuyafuata hayo watoto wetu watateseka yoyoooo!

    Halafu kuna huu ubeti sijaupata vizuri bado.

    "Enyi wake za watu punguzeni vitukooo,
    nasema punguzeni kwani si halaliii, je niambie wewe mke wa mtu hutembea umalainika kama bamia na ....... mwilini, unataka nini weweee?

    Dudumizi kwa kutongoza alikuwa ninja kweli. RIP, Jerry!

    Mze Kitime kaza buti baba tuletee burudani japo wewe ni jeshi la mtu mmoja lakini tuko nawe.

    ReplyDelete
  7. Namuunga mkono Seneta wa Msondo hapo juu. Ni kweli kuna wanamuziki wa kizazi kipya ambao sauti zao zinafaa sana kwenye muziki wa dansi. Miongoni mwao ni Marlaw, Q Chilla, Bushoke na Suma Lee. Hawa ingefaa wafuate nyayo za Lady Jay Dee na Banana Zorro kupiga muziki wa dansi 'live' jukwaani.

    ReplyDelete
  8. Kitime wewe ni mkombozi wa muziki wa Tanzania. Sikutegemea hata siku moja kuona muziki wa zamani wa Tanzania ukipigwa live ndani ya YouTube. Hii ni lulu halafu kinachonimaliza ni quality ya hii video. Ni ya hali ya juu sana ukilinganisha na mwaka iliyorekodiwa. Kama sikosei hii imepigwa kati ya mwaka 1991 na 1993 baada ya kifo cha Maneti pale Vijana Social Hall, Kinondoni. Ah! Jerry Nashon, Shaaban Yohana 'Wanted', Mohamed Salum 'Gotagota', Abdallah Mgonahazelu, Manitu Mussa...man! This is pure gold.

    ReplyDelete
  9. Ha ha haaaa! Shabani 'Wanted' hana budi kuiona hii huko aliko Botswana. Nina hakika itamkumbusha mbali sana mkali huyu wa solo. Hii inanikumbusha Vijana Day pale Kinondoni. Kwa waliotangulia mbele ya haki kama Maneti, Dudumizi na Gotagota Mungu aziweke roho zao mahali pema peponi. We miss you guys.

    ReplyDelete