Monday, September 19, 2011

Maelezo zaidi kuhusu Mzee Frank Humplink toka kwa mdau

Ili kukusaidia, hii hapa listi ya nyimbo za Frank na dada zake-: Mdudu, Mpenzi Rudi, Bibi Maria, Ua langu Jasmin, Keri Lochi, Efokulele, Sheikh Nuhu, Mama Pendo, Chiriku, Mama Sofia,Tupendane Wote, Niliona Chipukizi, Ukiwa Mtoto, Harusi ya Tausi, Show Me The Way Home, Nakupa Kwaheri,Niezoea Kusafiri, Siku Ya Kwanza, Hodi karibu, Hadijy, Sisi Kwa Sisi.
Kuna nyingine nyingi tuu lakini sijapata fursa ya kufanya utafiti. niko katika matayarisho ya kuandika kitabu kuhusu muziki wa Tanzania na panapo majaaliwa ya mungu tutafufua zaidi ukweli na haki ya wanamuziki kama kina mzee Frank. Kwa ufahamisho tuu, ule wimbo wa Western Jazz 'Nilikupenda sana' umesajiliwa kama utunzi wa Juma Mzingo wa Safari Sound. Tutaaamka lini?


Hamissi Delgado

3 comments:

  1. Tatizo ni kuwa sisi wasanii km wanamuziki,wanamichezo nk wa Tanzania ni wavivu wa kutunza kumbukumbu pia wavivu wa kufuatilia habari,na ndiyo maana habari nyingi kuhusu muziki,michezo na sanaa kwa ujumla zihusuzo Tanzania zimepotea na wahusika kuonekana kukata tamaa na maisha kwa kutojali wala kufuatilia historia yoyote inayohusu shughuli hizi za sanaa.Mimi binafsi namshukuru sana ndugu Kitime kwa ujasiri wake wa kuzisaka habari za muziki ambazo nadhani bila yeye zilikuwa zinazidi kuangamia,Jambo jingine linalochangia kwanza kuumaliza muziki hasa wa dansi Tanzania na kuupoteza kabisa ni huu utitiri wa stations zetu za redio zilizozagaa kila upande wa nchi na hasa hapo Dar,unakuta mtagazaji tangu aanze kazi ya utangazaji anajua bongo fleva tu,ukimuuliza Mbaraka Mwinshehe,Marijan Rajab,Wema Abdallah,Ahmaed Kipande.Mwinamila,Mzee Makongoro nk.,hajui kabisa,na hawa ndio wanaonekana mastaa kabisa ktk redio zetu,Tujue kuwa media ndicho chombo kinachotangaza mambo yote iwe utamaduni,siasa na maisha ya binadamu kwa ujumla,ipo haja ya kuzielimisha hizi redio za kizazi hiki kuwa open minded na siyo kulalia upande mmoja,huu unakuwa siyo utangazaji bali ni ushabiki.Watangazaji hawa chipukizi inabidi pia wasome historia ya sanaa ya nchi kwa ujumla na siyo kutangaza tu kama kasuku na kupata sifa za mitaani,Tujitahidi kufuatilia habari zote za sanaa yetu ili wasanii wengine eg.wa nchi jirani wasichukue haki miliki zetu kwa urahisi na sisi tukiwa tumezubaa tu. Abbu Omar,Prof.Jnr(Mwanamuziki)Tokyo,Japan.

    ReplyDelete
  2. Nakubaliana na Abuu. Tatizo si katika muziki na sanaa tu. Tatizo la kuhifadhi kumbukumbu za utamaduni wa taifa liko katika nyanja nyingi. Napendekeza yafuatayo: (1) Wizara ya Utamaduni iombwe ushauri wake kabla ya majengo yaliyoorodheshwa ("gazetted") hayajavunjwa. Officers' mess za kwanza za wajerumani na ya waingereza (Salamander zimekwishavunjwa na kuna fununu kuwa jengo la kiwanda cha kwanza cha sabuni Afrika Mashariki na Kati huendwa likavunjwa hapo Kisutu uhindini)(2) Alama na matangazo maalum yawekwe katika kumbukumbu za taifa (national monuments) k.m. askari monument, clock tower ya Samora Ave. n.k. (3)Pamoja na hali ngumu ya uchumi dunia nzima, bajeti ya serikali iongezwe katika nyanja zifuatazo: (a)nyaraka za taifa (national archives), (b)idara ya mambo ya kale (division of antiquities) (c) utafiti wa mila na desturi (ambayo itatumika kurekodi na kutunza kumbukumbu za za kihistoria za wasanii, wanamichezo na historia kwa jumla) (d) mabaraza yaliyo chini ya Wizara ya Utamaduni yaongezewe ruzuku kufanyia kazi ya utafiti na utunzaji wa kumbukumbu. Mabaraza hayo ni Baraza la Sanaa, Baraza la Michezo na Baraza la Kiswahili. Namalizia kwa kumnukuu Malcolm X "We have to know where we are coming from in order to know where we want to go".

    ReplyDelete
  3. Safi sana, nimeelimika sana kwa kusoma habari za Frank kwa mara ya kwanza..hongera sana kwa ufafanuzi mzuri.

    ReplyDelete