Sunday, August 21, 2011

Malaika wimbo wenye utata

Fadhili Wiliam anaetambulika kama mtunzi wa wimbo Malaika
Kuna nyimbo nyingi duniani ambazo zimekuwa na utata kuhusu aidha utunzi au upigaji wake. Kwa mfano kumekuwa na hadithi nyingi kuhusu kundi la Bonny M kuwa nyimbo zao zile hazikuwa zinaimbwa na wao, na hasa ile sauti ya mwanaume  aliyeimba studio alikuwa ni producer wao. Kulikuweko na kundi la Nili Vanili ambalo licha ya kutoa album kadhaa zilizotikisa ulimwengu ilikuja dhihirika kuwa waliokuwa waliokuwa wanarekodi nyimbo hizo ni watu wengine kabisa na waliokuwa wanaonekana kwenye cover ya album, siri ilipovuja ukawa mwisho wa kundi hili. Hapa kwetu kuna utata ambao sijui kama utakuja pata jibu, nao ni kuhusu utata wa nani mwenye wimbo wa Malaika. Hadithi moja ni kuwa mtunzi halisi wa wimbo Malaika alitoka Moshi na alikuwa kamtungia mpenzi wake. Lakini pamoja na kuwa aliutunga na ukawa unapigwa 'live' hakuurekodi. Ila Fadhili William ambae inadaiwa wakati huo alikuwa fundi mitambo wa bendi alikuja kuurekodi na kuusajili kama ni wake na hivyo kupata fedha nyingi sana kutokana na wimbo huo.

1 comment:

  1. Kuhusu wimbo wa MALAIKA muone Mzee ALLY SYKES ndiye anayejua hasa mtunzi wa wimbo huu.

    ReplyDelete