Kwa wale waliokuwa wapenzi wa RTD watakumbuka kipindi kilichokuwa Jumapili asubuhi ambapo RTD ilitembelea hospitali mbalimbali na kuwawezesha wagonjwa watume salamu. kipindi kiliitwa 'Salamu za wagonjwa'. Wimbo ulioashiria kuanza na kuisha kwa kipindi hicho ulipigwa na mwanamuziki Mzee Kungubaya nimebahatika kupata tena picha yake huyu ndiye Kungubaya. Angalia hiyo stika kwenye gitaa mnakumbuka CO CABS?
mzee kungubaya yupo kibaha maili moja kwa sasa ni jirani yangu,mara nyingi humuona akikata mitaa na gitaa lake kwenye ma bar na ukimpa chochote anakupigia muziki,
ReplyDeletedu! hapa pa kupiga gitaa bar ndipo alipofikia ilhali RTD wameutumia wimbo wake kwa miaka mingi sana mpaka hivi karibuni
ReplyDeleteSelikali inatakiwa kuweka mikakati mizuri ya muziki Wa Tanzania ili wanufaike na jasho lao
ReplyDeleteWimbo nani anao?
ReplyDelete