Sunday, August 21, 2011

Chinyama Chiaza aka Chichi

Kushoto Chinyama Chiaza, kushoto Chibangu Katai(Mzee Paul)
Chinyama Chiaza alikuwa si tu mpuliza saxaphone mahiri bali alikuwa kiongozi mzuri sana. Aliiwezesha Orchestra Maquis Du Zaire kuingia katika biashara na wakati huo kuanzisha kampuni-Orchestra Maquis Company iliyojulikana zaidi kama OMACO, ambapo bendi hiyo iliweza kuwa na mashamba, sehemu ya kuuzia mazao Kariakoo na hata nyumba kadhaa za bendi eneo la Sinza mkabala na shule ya Mashujaa Sinza. Kifo chake 1985 kiliiyumbisha sana Maquis, kuna wengi wanaoona kuwa kifo cha Chichi ndicho kilichoanzisha kuporomoka  kwa Maquis

1 comment:

  1. Hongera kwa kuteleta historia fupi ya kundi la Orchestra Maquiz du Zaire.Naomba ukipata nafasi tuelezee zaidi

    ReplyDelete