Tuesday, March 22, 2011

Mwaka wa misiba kwa wanamuziki Tanzania




Bi Mwanahawa baada ya ajali
Wanamuziki 13 wa kikundi cha Five Star Modern Taarab wamepoteza maisha katika ajali ya gari ambapo basi lao dogo  liligonga gari lililokuwa limepark kando ya barabara. Ajali hiyo mbaya ya wanamuziki wengi kufa kwa pamoja inaweza ikafananishwa na ile ajali ya miaka ya 70 ambapo bendi nzima ya Njohole Jazz nayo iliangamia katika ajali ya gari. Wanamuziki walikwisha tambuliwa mpaka sasa ni Issa Kijoti, Nasoro Madenge, Fembe Juma, Omary Hashim, Omary Tall, Tizo, Mapande, Ngereza Hassan, Hamisa Omari, Maimuna, Haji Msaniwa. Muimbaji maarufu bi Mwanahawa Ally ni mmoja wa wanamuziki walionusurika katika ajali hiyo.

1 comment:

  1. Ni ujinga ulioje kuhusisha ajali hii na mambo ya ushirikina. Ajali hii ilisababishwa na uzembe wa dereva ambaye alikuwa akiendesha kwa kasi bila ya kuwa mwangalifu, kwa mujibu wa walionusurika.

    ReplyDelete