Tuesday, March 22, 2011

Mwaka wa misiba kwa wanamuziki Tanzania 2

Mwanamuziki wa siku nyingi, ambaye amewahi kupigia bendi kama Maquiz, OSS, Diamond Sound, na kwa sasa alikuwa Wazee Sugu akishiriki kama mpiga tumba Gulukulu Abandoki Tomaa amefariki leo saa sita na nusu mchana (22/3/2011), katika hospitali ya Mwananyamala. Mtoto wa mwanamuziki huyu, Alphonse aliwahi kupigia drums bendi ya Akudo. Taarifa za mazishi zitafuata. Mwanamuziki huyu aliwahi kupata sifa ya pekee pale ambapo alichaguliwa  na Tabu Ley alipokuja Tanzania na kuweza kufanya nae maonyesha katika miji mbalimbali Tanzania kama mpiga tumba wa Afrisa International. Motoo alimwomba Tabu Ley ampe lifti katika ndege yake wakati wa kurudi Kinshasa. Alipofika huko inasemekana alishindwa kupata wenyeji na hasa pale Tabu Ley alipomuacha bila kumchukua katika bendi yake. Kwa njia moja au nyingine Motoo alirudi tena Tanzania ambako ameishi mpaka mauti yamemkuta

3 comments:

  1. John, Poleni sana and please extend my condolences to families of the deceased

    ReplyDelete
  2. Natoa pole sana kwa familia ya mwanamuziki ndugu yetu Motoo,huyu pia aliwahi kupitia bendi ya Simba Wanyika Nairobi miaka ya nyuma,mungu aiweke roho yake pahali pema peponi.
    Abbu Omar,Prof.Jnr(Mwanamuziki)Tokyo,Japan.

    ReplyDelete
  3. Namkumbuka Motoo. Mara ya mwisho nilimuona akiwa na OSS ukumbi wa IFM. Nakumbuka upigaji wake wa tumba na tabia yake ya ukimya, weusi wake na macho yake mekundu sana.

    Nikiwa Gothenburgh, Sweden miaka 3 iliyopita nilimuulizia Motoo kwa mwanamuziki mmoja wa Kizaire akaniambia jinsi Motoo alivyorudi Kongo na jinsi alivyorudi Tanzania. Yalikuwa mazungumzo yaliyoambatana na bia halafu jioni jua likiwa linazama. Stori nzima na set up tuliyokuwepo ilifanya madhari yote kuwa ya huzuni.

    Motoo umewafuata wapiga tumba wenzako kina Sidi Moris na William "Kizibo" Chiduo. Pumzikeni kwa Amani. Amen.

    ReplyDelete