Thursday, February 27, 2014

ORCHESTRE SANTA FE ILIKUWA BENDI YA KWANZA YA WAKONGO WATUPU NCHINI?

Kati ya maswali amabayo yamewahi kuulizwa humu ni kuhusu bendi hii Orchestra Santa Fe. Hii ilikuwa mwanzo ni bendi yenye asilimia kubwa ya wanamuziki Wakongo. Kuna wakati Blogger Kiongozi Issa michuzi aliwahi kuuliza kama Je,Sante Fe ndio ilikuwa Bendi ya kwanza ya Kikongo? Sina jibu bado kuhusu hili. Wenye taarifa zaidi kuhusu Bendi hii karibuni. Bendi hii ilikuwa ikipiga pale Gateways Mnazi Mmoja maeneo ambayo kuna wakati yalikuwa maeneo muhimu katika shughuli za starehe jijini Dar es Salaam.Kuna maoni yaliwahi kutoleaa kuhusu mada hii katika blog iliyokuwa kabla ya kuzaliwa hii na haya ndio yalikuwa maelezo yao:

      1. BLACKMANNEN said...
Orchestra Santa Fe, haikuwa ya Wakongo. Bendi za Fouvette na akina "Papa Mikey" ndiyo waliokuwa Wakongo wa mwanzo Tanzania.

Orchestra Santa Fe, Tanzania Jazz Band, King Africa Jazz Band na Orchestra Quilado zote zilikuwa za Kitanzania, ila habari zake wengi hatuzijui.

It's Great To Be Black=Blackmannen
2. 
Anonymous said...
TP SANTA FE ILIKUWA NI BENDI YA WAKONGO ILINGIA NCHINI IKITOKEA ZAMBIA NA BAADHI YA WANAMUZIKI WA ZAMBIA MMOJA WAPO NI MPIGA BASS JOSEPH MULENGA,WAKATI TP SANTA FE INAPIGA GOROFA YA TANO GATE WAYS SAFARI TRIPPES ILIKUA ATUA CHACHE PRINCESS BAR KUNA SIKU MPIGA BASS WA TRIPPERS MAREHEMU CHRISTIAN KAZINDUKI ALIPATA AJALI YA PIKIKI PALE KONA YA CENTRAL POLICE KUKAWA HAKUNA MPIGA BASS ILIBIDI MASHABIKI TUTOKE KWENDA KUMUZIMA MULENGA ILI DANSI LETU LIPIGWE NANDIO UKAWA MWANZO WA NYOTA YAKE KUNG'AA ALIJIUNGA NA TRIPPERS NA NYIMBO YAKE YA KWANZA KUREKODI MATESO DHIKI NA MATESO AKIPIGA RIDHIM GITAA ,ABDALA GAMA SOLO,BENNY PETTY SECOND SOLO,KAZINDUKI BASS,KABLA YA KUHAMIA DAR INTERNATIONAL NA KUKUTANA NA MZAMBIA MWENZI MKUBWA WAKE MICHAEL ENOCK ALIE MTRAIN KUWA MPIGA SOLO SIKILIZA NYERERE BABA MLEZI NYERERE MWANA MAPINDUZI THEN AKAENDA SIKINDE.

1 comment:

  1. Baada ya post hii kuonekana Facebook mwanamuziki wa zamani Mzee Kasongo Wa Kanema ameandika hivi...... tazama kwenye mike mbele ya Wabangoi ni mimi nimeshushumaa ihi ndio band ili nileta east africa hapa kabla sija join Maquis du Zaire Sax Mzee Matu Jean , guitare milongo, joseph mulenga, dovin luboya.na hapa ni gate way mnazi mmoja kwa mzee Simkoko.nakumbuka ,wewe una library nimeamini.

    ReplyDelete