Jeff kwa sasa yuko Mlimani Park Orchestra |
Upanga
ni eneo muhimu sana katika historia ya muziki Tanzania. Hata katika
miaka ya karibuni kulizuka kilichoitwa East Coast, muungano fulani wa
wasanii wa Bongoflava toka maeneo ya Upanga, hii haikuwa mara ya kwanza
kwa Upanga kuwa na wanamuziki waliotingisha mji. Enzi hizo za muziki wa
soul, vijana wa Upanga walilipa eneo hili la mji jina la
Soulville.Kwenye kona ya barabara ya Mindu na United Nations, nyumbani
kwa familia ya Jengo, hapo ndipo palikuwa mahala pa mazoezi pa kundi
lile la Groove Makers.
Baadhi ya wanamuziki wa kundi hili walikuwa Mohamed Maharage, Joseph
Jengo, Emmanuel Jengo, Herbert Lukindo, Willy Makame, na mpiga Drums
ambae mpaka leo yupo katika anga za muziki Jeff. Kipindi hiki kilikuwa
ni wakati wa muziki wa soul na kundi hili lilikuwa kundi la ubora wa juu
wakati huo. Upanga ilikuwa na kundi jingine The Strokers,
hili lilikuwa na awamu mbili, awamu ya kwanza ilikuwa na wanamuziki
akina Donald Max, David Max, Harry Chopeta, Vincet Chopeta, Pino Makame
na Ochiwa na Freddy Lukindo.
Awamu
ya pili ya kundi hili lilkuwa na Sajula Lukindo,Onesmo Kibira,Innocent
Galinoma,Ben Galinoma, Denis Pad,Francis Kasambala,Vicent na Harry
Chopeta, Ally Mwarabu, Sabri Mmanga na wengineo. Barlocks ni Bendi nyingine i
liyochipukia Upanga, jina la Barlockslilitokana na kuweko kwa kundi laBarkeys ambalo leo linaitwa Tanzanites.Barlocks walikuwa wakitumia vyombo vya Barkeys kwani kwa wakati huo bendi hizi zilikuwa kama mkubwa na mdogo. Barlocks hiyo
ya awamu ya kwanza ilikuwa na wanamuziki akina Jimmy Jumba,Pimbi
Sokoine, huyu alipewa jina la utani Pimbi kutokana na kuwa mrefu sana,
Said Mbonde kaka yake Amina Mbonde mwanamuziki mwingine muimbaji,Sajula
Lukindo, Abraham. Kulikuweko na makundi mengine mengi hapo Upanga, kamaWhite Horse, Aquarius hapa
walikuweko producer maarufu Hendrico Figueredo, Joe Ball,Joel De Souza,
Mark De Souza,Roy Figueredo, Yustus Pereira,Mike De Souza. Baadhi ya
wanamuziki wake walienda na kuungana na wengine Arusha na kuvuma sana na
kundi la Crimson Rage, baadae wakarudi Dar na kujiita Strange. Baadhi ya kumbi walizokuwa wakipiga zilikuwa DI, Marine,Gymkhana,Maggot, St Joseph na kwenye shule mbalimbali.
(Picha
ya juu-Emmanuel 'Emmy' Jengo, Joseph 'Joe' Jengo, Herbert 'Herby'
Lukindo. Kati-Jeff 'Funky' nyuma yake ni Willy Makame. Picha ya chini
Willy Makame)
No comments:
Post a Comment