Chakachua ndio ulikuwa mtindo wao, walikuwa na mpiga solo ambae wapiga
magitaa wote waliomjua wanamheshimu kwa upigaji. Kuna mwanamuziki
Mtanzania aliyeko Japan Abbu Omar, aliwahi kunambia kuna siku aliwahi
kumsikilizisha muziki wa Chakachua mpiga gitaa mahiri George Benson,
George Benson alisikitika sana kusikia aliepiga gitaa vile ameshafariki
kwani alitaka wakutane watengeneza kitu cha pamoja, huyu si mwingine
bali ni Michael Vicent. Na bendi ilikuwa Urafiki Jazz iliyokuwa chini ya
Kiwanda cha nguo cha Urafiki Dar Es Salaam...ENDELEA HUKU
No comments:
Post a Comment