Monday, April 1, 2013

TWISTI NI PENDO LANGU, PENDO LANGU LA MOYONI

WAU WAU WAU X2
TWISTI NI PENDO LANGU
PENDO LANGU LA MOYONI
WASICHANA WA KALOLENI
WALINICHEZEA VIZURI SANA
MWANAMUZIKI CHUBBY CHECKER NDIE AMBAYE HUPEWA SIFA YA KUIENEZA TWIST DUNIANI, NA HASA BAADA YA KIBAO CHAKE 'THE TWIST' KUWA KATIKA TOP TENA ZA BILLBOARD 1960, BAADAE ALIPOROMOSHA VIBAO VINGI VYA MTINDO HUO KIKIWEMO LETS TWIST AGAIN. WANAMUZIKI WALIOKUWA NAIROBI KATI YA MIAKA 1964 NA 1966 WALIREKODI NYIMBO NYINGI SANA ZA TWIST AMBAZO HUPENDWA SANA MPAKA MIAKA YA LEO. DAUDI KABAKA AMEWAHI HATA KUPEWA JINA LA MFALME WA TWIST YA KENYA KUTOKANA NYIMBO NYINGI ZA TWIST ALIZOZIREKODI IKIWEMO AFRICAN TWIST, TAITA TWIST,BUSHBABY TWIST, BACHELOR BOY TWIST, NA HATIMAE NYIMBO KAMA HARAMBE HARAMBE. BENDI NYINGI HUKU KWETU PIA ZILIPIGA MUZIKI HUU WA TWIST BILA KUMSAHAU SALUM ABDALLA NA CUBAN MARIMBA WALIOPIGA STAILI NYINGI SANA IKIWEMO TWIST, NA HATA TUKAWA NA BENDI KULE MWANZA IKITWA KIMBO TWIST BAND.

1 comment:

  1. Hapa ktk story ya huyu mpiga gitaa wa Air fiesta ya kusahau hata nyimbo alizotunga mwenyewe na pia kukana kuweko ktk shughuli hizi za miziki,nimecheka sana badala ya kusikitika,hii inatufundisha na kutuonya kuwa madawa hata pombe huvuruga kabisa maisha ya wanamuziki hata kupelekea vifo,Inabidi tuwaonye watoto wetu wasifuate nyayo hizo kabisa,kwani ulevi wowote ni adui wa maendeleo na maisha ya mwanadamu.

    ReplyDelete