Friday, March 22, 2013

African Influence-bendi ya wakongwe



JOHHNY ROCKS

NURUDIN OMARY

Katika bahati moja niliyoipata ni kugundua kiota kimoja ambacho wanamuziki wakongwe watatu wamejikusanya na kuanza kupiga muziki ambao ni wa hali ya juu na hivyo kujipatia mkataba wa kupiga kwa masaa mawili pale Holiday Inn katikati ya jiji la Dar es Salaam. Wanamuziki hawa wakiongozwa na mkongwe mwenzao Johnny Rocks mpiga drum mwenye historia ya muziki inayoanzia miaka ya 60, walikuwa wakipiga nyimbo mbalimbali kutoka pande zote za dunia, Jazz, Rock n Roll, Blues na hivyo nikapata nafasi ya kusikia nyimbo kama Love me tender, Take 5, Quando quando ambazo sijazisikia zikipigwa 'live' kwa ufasaha kwa miaka mingi

No comments:

Post a Comment