|
Hodi Boys |
|
Slim Ally |
|
Sal Davis |
|
Steel Beautah |
-->
Kama ulikuwa kijana miaka ya
70 lazima ulikuwa unaifahamu ile miamba ya muziki wa funk iliyokuwa ikiwika
nchini Kenya. Steele Beauttah, Kelly Brown, Slim Ali, Ishmael Jingo na wengine
wengi. Katika ukumbi wa Starlight Club katikati ya jiji la Nairobi uliofunguliwa
rasmi May 15 1965, mwenye ukumbi huo Robbie Armstrong aliwezesha ukumbi
kuingiza kasi cha watu 12,000 kila mwezi kwa kuzikaribisha bendi zilizokuwa
kali kama The Ashantis, Air Fiesta Matata, The Cavaliers, kufanya maonyesho
katika klabu hiyo. Wanamuziki wa bendi hizi waliiga ‘swaga’ za mwenyewe
Godfather of Soul marehemu James Brown, uvaaji utanashati na hatimae uimbaji,
kati ya wanamuziki wa kwanza kuwa wafuasi wa JB alikuwa ni Salim Abdullah Salim
ambaye tunamfahamu kwa jina la Sal Davis ambaye vibao vyake kama Unchain my
heart, Makini akili vilitikisa sana anga za Afrika mashariki miaka ya 60.
Huwezi kuacha kumtaja Kelly Brown mwanamuziki mwingine wa Kenya ambaye alihamia
Ujerumani na kuishi huko mpaka kifo chake 1989. Muziki wa Boogie ndio ulitawala kwa vijana huu ulikuwa muziki
uliopigwa mchana kuanzia saa nane hadi saa 12 jioni. Viongozi wengi hawakupenda
Boogie kwa madai kuwa linaharibu vijana, na pia mitindo ya mavazi na swaga za
wakati huo ziliongeza wasiwasi wa
viongozi hawa, vijana wakiwa na viatu vya raizon, nywele kwa mtindo wa
Afro, suruali za bell bottom , na mashati ya kubana mtindo wa slim fit
vilikosesha sana usingizi wazee. Lakini muziki uliopigwa wakati huo ulikuwa ni
wa hali ya juu sana, kibao kama You can do it cha Slim Ally au Fever
iliyotungwa na Ishmael Jingo ni ushahidi tosha. Bahati mbaya wanamuziki wake
walipotea mmoja mmoja na wengine kufa vifo vya kudhalilika katika umasikini.
Steele alikuwa bandleader wa
kundi la Air
Fiesta Matata. Kundi hili lililokuwa na wanamuziki 10, lilikuwa bingwa wa
muziki wa funk kiasi cha kuweza kupiga na Miles Davis 1969, na alilipenda mpaka
alilialika kundi zima kwenda kupiga nae Marekani. Mwaka 1971 BBC World service
ililitaja kama bendi bora Afrika. Steele alianza madawa ya kulevya kama walivyoanza
wanabendi wenzie baada ya kupata tour ya kuzunguka ulimwengu 1974. Bendi
ilianza kwa kwenda Hong Kong, kasha Uswisi na Uingereza. Wakati wakiwa tayari
kwa safari ya kurudi Kenya wakiwa
na vyombo vipya na vizuri meneja wao Mogosti akawaambia ana tatizo la viza kwa
hiyo watangulie yeye atawafuata Kenya kwa ndege iliyokuwa inafuata. Hakuonekana
tena, naye ndie alikuwa na fedha na vyombo, ilisemekana alihamia Jamaica, Air
Fiesta Matata ikavunjika baada ya hapo. Tatizo la madawa ya kulevya
lilimuandama Steele kiasi cha kuamua kufa kwenye mtaro wa maji machafu lakini
wanae walimuokota na kumsaidia baada ya muda akaokoka. Mpiga gitaa wa Matata
Sammy Kagenda naye pia alidhurika na madawa aina ya heroine kiasi cha
kutokukumbuka hata nyimbo alizotunga mwenyewe, na hata alipoonyeshwa picha zake
akiwa kwenye maonyesho alikana kuwa hakumbuki kuweko katika shughuli hiyo.
YOU CAN DO IT
FEVER
MAKINI
No comments:
Post a Comment