|
Emmanuel 'Emmy' Jengo, Joseph
'Joe' Jengo, Herbert 'Herby' Lukindo. |
|
Jeff 'Funky' |
|
Willy Makame |
Upanga ni eneo muhimu sana
katika historia ya muziki Tanzania. Hata katika miaka ya karibuni kulizuka
kilichoitwa East Coast, muungano fulani wa wasanii wa Bongoflava toka maeneo ya
Upanga, hii haikuwa mara ya kwanza kwa Upanga kuwa na wanamuziki waliotingisha
mji. Enzi hizo za muziki wa soul, vijana wa Upanga walilipa eneo hili la mji
jina la Soulville.Kwenye kona ya barabara ya Mindu na United Nations, nyumbani
kwa familia ya Jengo, hapo ndipo palikuwa mahala pa mazoezi pa kundi lile la Groove
Makers. Baadhi ya wanamuziki wa kundi hili walikuwa Mohamed Maharage,
Joseph Jengo, Emmanuel Jengo, Herbert Lukindo, Willy Makame, na mpiga Drums
ambae mpaka leo yupo katika anga za muziki Jeff yuko katika kundi la Mlimani Park Orchestra. Kipindi hiki kilikuwa ni
wakati wa muziki wa soul na kundi hili lilikuwa kundi la ubora wa juu wakati
huo. Upanga ilikuwa na kundi jingine The Strokers, hili lilikuwa na
awamu mbili, awamu ya kwanza ilikuwa na wanamuziki akina Donald Max, David Max,
Harry Chopeta, Vincet Chopeta, Pino Makame na Ochiwa na Freddy Lukindo. Awamu
ya pili ya kundi hili lilkuwa na Sajula Lukindo,Onesmo Kibira,Innocent
Galinoma,Ben Galinoma, Denis Pad,Francis Kasambala,Vicent na Harry Chopeta,
Ally Mwarabu, Sabri Mmanga na wengineo. Barlocks ni Bendi nyingine iliyochipukia
Upanga, jina la Barlocks lilitokana na kuweko kwa kundi la Barkeys
ambalo leo linaitwa Tanzanites. Barlocks walikuwa wakitumia
vyombo vya Barkeys kwani kwa wakati huo bendi hizi zilikuwa kama mkubwa
na mdogo. Barlocks hiyo ya awamu ya kwanza ilikuwa na wanamuziki akina
Jimmy Jumba,Pimbi Sokoine, huyu alipewa jina la utani Pimbi kutokana na kuwa
mrefu sana, Said Mbonde kaka yake Amina Mbonde mwanamuziki mwingine
muimbaji,Sajula Lukindo, Abraham. Kulikuweko na makundi mengine mengi hapo
Upanga, kama White Horse, Aquarius hapa walikuweko producer
maarufu Hendrico Figueredo, Joe Ball,Joel De Souza, Mark De Souza,Roy
Figueredo, Yustus Pereira,Mike De Souza. Baadhi ya wanamuziki wake walienda na
kuungana na wengine Arusha na kuvuma sana na kundi la Crimson Rage,
baadae wakarudi Dar na kujiita Strange. Baadhi ya kumbi walizokuwa
wakipiga zilikuwa DI, Marine,Gymkhana,Maggot, St Joseph na kwenye shule
mbalimbali.
Umesahau kundi lingine baada ya hayou
ReplyDeleteAmbalo lilikuwa na marehemu eddy..Marehemu madaraka masumbigana..martin