Siti Binti Saad |
Kwa
kila hali Siti Binti Sadi anastahili kuenziwa. Kwa akina mama, mwanamke
huyu shujaa aliyetoka katika familia maskini ya kijijini, ataenziwa kwa
kuwa aliweza kushinda mfumo uliokuwa ukizuia wanawake kujichagulia
mfumo wa maisha yao, na kuweza kujitokeza kufanya yale ambayo
hayakuwezekana kwa mwanamke wa aina yake kabla. Alijitokeza na kuwa
mwanamke mwimbaji mwenye nguvu za kuendesha shughuli za muziki katika
mfumo uliotawaliwa na wanaume.
Kwa akina mama wanamuziki katika Taarabu, alikuwa ndio ufunguo ya mfumo uliopo ambao taarab inaongozwa na waimbaji wa kike.
- Alikuwa ndie mwasisi wa kuimba taarab kwa Kiswahili.
Kwa wanamuziki wote kwa ujumla Siti Binti Sadi ni super star wa kweli.
- - Alirekodi santuri zaidi ya 150
- - Alikuwa wa kwanza kwenda kurekodi nyimbo zake India May 1928
- - Umaarufu wake ulisababisha Columbia Records kujenga studio Zanzibar katika enzi yake ili tu kumrekodi.
- Oktoba
1936 aliwahi kufanya onyesho moja huko Pangani na kupata shilingi 1200.
Kwa thamani ya pesa wakati ule, mtu aliweza kupanga chumba kwa shilingi
1 kwa mwezi. Na Pangani ilikuwa na wastani wa watu 1500. Si rahisi
msanii yoyote wa leo hapa nchini kuweza kufikia Usuper Star huo. Ni kama hivi Dar ina wakazi milioni nne we uweze kufanya onyesho waingie zaidi ya aslimia 75 ya wakazi, kitu kama watu milioni 3. Huku ndio kutetemesha jiji kwa kiukweli.
Siti alizaliwa mnamo mwaka 1880 na kufariki 1950.
No comments:
Post a Comment