Kwa
muda mrefu nilikuwa na nia ya kuweka taarifa kuhusu wimbo wa kumsifu
Nyerere ambao uliimbwa na Mheshmiwa Paul Kimiti. Nilijitahidi kutaka
kupata taarifa kutoka kwake ikawa haikuwezekana lakini karibuni nilisoma
maelezo ya Mheshimiwa mwenyewe kuhusu kazi hiyo, ambayo alisema alifanya akiwa Mwenyekiti wa wanafunzi kutoka Tanganyika katika chuo
kikuu cha Netherlands kati ya mwaka 1962 na 1965. Akiwa na wanamuziki
wenzake wakiwa na kundi waliloliita Safari Brothers walirekodi nyimbo
hii nzuri sana kuhusu Mwalimu Nyerere. Mheshimiwa alisema walitoa dola
20,000 walizozipata kutoka Philips records kwa Mwalimu alipotembelea
Netherlands April 1965, pesa hizo walitoa ili kuchangia maendeleo ya
nchi yetu, na huo ndio ulikuwa mwanzo wa uhusiano wake na Mwalimu.
No comments:
Post a Comment