Sunday, June 24, 2012

Salamu kutoka kwa Nguza Viking


Nguza enzi za Maquis na mtindo wao wa Scania LBT
Nimekwenda gereza la Ukonga asubuhi hii kumsalimia Nguza na mwanae Papii, nimewakuta wachangamfu wenye afya nzuri. Nguza kanituma NIWASALIMIE WOTE, naomba nitumie jukwaa hili kutangaza salamu hizo. Ni wazi italazimika kuomba muda wa ziada kutoka kwa uongozi wa Magereza kuzungumza zaidi na Nguza, jambo mojawapo ambalo tutalizungumza ni kuhusu mapato ya wimbo wa Seya. Pamoja na umaarufu wote ni jambo la kusikitisha kuwa Nguza anasema hajapata fedha yoyote kutoka wimbo ule, zaidi ya fedha alizopewa kuingia studio kuurekodi. Swali ni nani anazipokea fedha za wimbo ule?

Papii na Nguza

1 comment:

  1. John, ahsante sana kwa huu ujumbe. Hi kweli inasikitisha. Anyways sasa tufanye nini cha kuweza kuwasaidia Papi na Nguza wapate haki zao. Mimi niko tayari kusaidia kwa hali na mali

    ReplyDelete