LaDonna Adrian Gaines aliyejulikana zaidi kwa jina la Donna Summer amefariki leo
Key West Florida akiwa na umri wa miaka 63. Donna Summer amefariki kwa tatizo
la Kansa. Donna alizaliwa tarehe 31 December 1948.
LaDonna alikuwa mmoja wa
watoto saba katika familia yao iliyokuwa inaishi Boston, Marekani. Mwaka 1971
Donna akahamia Austria ambapo alikutana na Helmuth Sommer ambaye walicheza wote
sinema ya Godspell, na wakaoana 1973 walipata mtoto mmoja lakini ndoa ilivunjika
1975. Donna alichukua jina la huyo mumewe aliyekuwa Mjerumani na kulitafsiri
jina kwa Kiingereza na akapata jina la Summer ambalo ndilo lilikuwa jina lake
la jukwaani. Mwaka 1978 wakati anatayarisha kibao cha ‘Heaven Knows’ ndipo
alipokutana na Bruce Sudano na wakaoana July 16, 1980, japo 1979 walipata mtoto
wao kwanza, mtoto wa pili alizaliwa 1981.
Pamoja na nyimbo zake kuigwa
na wanamuziki wengi kama Madonna, Whitney Houston, Diana Ross, Britney Spears, kwa mfano ule wa "Love to Love You Baby" ulikuwa sampled na Beyonce Knowles
na unajulikana kama "Naughty Girl", Donna alikuwa na rundo la awards
na mafanikio mengine, kati ya awards alizopata ni;
- NAACP Image Award
- Juno Award nomination kwa Best Selling International Single,"I Feel Love"
- Multi-Platinum album 3 katika Marekani
- Album zake 11 zilipata Gold nchini Marekani
- Gold singles 12
- American Music Awards 6
- Alikuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kupata MTV Video Music Awards
- Golden Globe Awards 2
- Donna Summer aliweza kupata jumla ya Grammy Awards 5
- Na aliwahi kuteuliwa mara 12 kwa ajili ya Grammy Award
Alipata heshima nyingine nyingi tu
Tulio cheza muziki wako tutakumiss Donna,
Nakumbuka Love to love you baby, Bad Girls, I feel love na
kadhalika
No comments:
Post a Comment