Monday, May 21, 2012

Robin Gibb wa BeeGees afariki dunia kwa kansa




Marehemu Robin Gibb
Baada ya kifo cha Donna Summer ( Desemba 31,1948-May 17, 2012), wiki iliyopita,ulimwengu wa muziki umepata pigo jingine baada ya Robin Hugh Gibb, mwanamuziki wa kundi maarufu la BEE GEES kufariki dunia Jumapili 20 May 2012, Robin  alizaliwa tarehe  22 Desemba mwaka 1949. 
Kundi la Bee Gees lilianzishwa kwa pamoja na pacha wake Maurice na kaka yao Barry, japo Robin ndie aliyekuwa maarufu zaidi katika kundi hili. Wazazi wao walikuwa Waingereza japo kwa kipindi fulani walihamia Australia. Inasemekana kundi hili ndilo lililokuwa na mafanikio kuliko kundi lolote jingine la Pop duniani. Kwa karibu miongo 6 kundi hili limekuwa jukwaani, likifanya maonyesho. Kundi liliweza kuuza zaidi ya santuri milioni 200.

 Watanzania wengi walianza kuwafahamu baada ya kusikia vibao vyao kama Staying Alive, Night Fever, How deep is your love na kadhalika  katika filamu ya filamu ya Saturday Night Fever. 

Tarehe 20 May 2012 Robin amefariki baada ya matatizo ya muda mrefu ya kansa ya utumbo. Pacha wake Maurice alifariki kw tatizo hilohilo 2003.

Grammy Awards ambazo kundi hili lilipata:

 1977 Best Performance by a Group — "How Deep Is Your Love"
1978 Best Performance by a Group — "Night Fever"
1978 Album of the Year — "Saturday Night Fever"
1978 Producer of the Year — "Saturday Night Fever"
1978 Best Arrangement of Voices — "Stayin' Alive"
2000 Lifetime Achievement Award
2003 Legend Award

No comments:

Post a Comment