Wednesday, January 11, 2012

Mzee Kipara afariki dunia

Marehemu Mzee Said Fundi-Mzee Kipara
Mzee Said Fundi, maarufu kama Mzee Kipara msanii ambaye amedumu katika sanaa kwa miaka mingi sana amefariki dunia asubuhi saa mbili leo Jumatano tarehe 11 Januari, 2012. Wengine tulimfahamu Mzee Kipara kwanza akiwa mwigizaji katika magazeti ya picha yaliyokuwa yakiitwa FILM TANZANIA, baadae kukutana nae 'live' akiwa  TT katika treni ya reli ya kati. Mzee Kipara pia alikuwa maarufu sana na sauti yake nzito ya kibabe katika michezo ya kuigiza ya redio ambayo ndiyo ilikuwa burudani ya maelfu ya Watanzania kwa miaka mingi. Mzee Kipara baadae alianza kuonekana na kujulikana sura zaidi pale alipoanza kuonekana katika michezo iliyoanza kurushwa katika TV,na baadae katika filamu kadhaa za Kitanzania. Mungu amlaze pema peponi, tunamshukuru Mungu kwa kutupatia hazina hii kwa miaka yote, Mungu alitoa na Mungu ametwaa.

No comments:

Post a Comment