Friday, October 21, 2011

Sogea Karibu wimbo wa Belesa Kakere akiwa JUWATA

Moja ya nyimbo za JUWATA ambazo zinaendelea kupendwa ni huu wimbo ambao ni utunzi wa Salehe Kakere 'Belesa' unaoitwa Sogea Karibu. Wimbo huu ulikuwa tofauti sana nyimbo za JUWATA wakati ule kwani ulitawaliwa na kinanda kilichopigwa na Waziri Ally 'Kisinger' inatamkwa Kisinja. Pia katika wimbo huu, hakuna vyombo vya kupuliza saxaphone na trumpets ambazo zilitawala kila nyimbo ya bendi hii wakati huo. 
Mshahiri yake haya hapa;

Belesa Kakere
Sogea karibu..nikueleze
Usije shangaa...imekuwaje
Upate fahamu ....na kuelewa
Kuwa ndoa yetu sasa....imevunjika
Nilikupeleka kwa wakwe zako ukaonane na ndugu zanguu
Hata mama yangu alifurahi sana
Na ndugu zangu walikupenda sanaa
Mapatano yetu dada ni kuoana
Kama tukitunza heshima yetu

Chorus
Sasa nasikia umefanya visa vingi
Hata mama yangu humthamini

Ikiwa mambo yenyewe ni hivyo,
Mbona mazito
Naona dada mimi ntashindwa,
Siwezi kukuoa tena.
Nilikueleza toka zamani kitu kimoja
Utunze heshima kwa wakwe zakoukapuuza,
Maji yaliyokwisha mwagika hayazoleki
Iliyobakia sasa majuto nenda kwenu kwa salama






6 comments:

  1. Bw. Kitime....hivi ninja kakele yupo wapi siku hizi na anafanya nini. Huyu jamaa alikuwa moto sana haswa pale alipohamia Bima Lee.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kwamba huu wimbo ilikuwa ni madongo kwa Mzee Gurumo?

    ReplyDelete
  3. siyo dongo kwa ngurumo,maana unasikia sauti yake humo,"ikiwa mambo yenyewe ni hivyo" siwezi kukuoa tena" Jk hivi huyu belesa kakere ndiyo juma kakere au ndugu?

    ReplyDelete
  4. KAKERE YUKO TANGA, NTAKUWA NA MAKALA YAKE KWENYE HII BLOG MUDA SI MREFU, NA WIMBO HUU HAUKUWA DONGO KWA GURUMO.

    ReplyDelete
  5. KAMA SIKOSEI NILIWAHI KUSIKIA SIKU HIZI NI MUAJIRIWA WA NSSF,NGOJA TUSUBIRI MAKALA KWA UNCLE KITIME TUTAJUA ZAIdi

    Seneta wa msondo,michigan,usa

    ReplyDelete
  6. Mzee Kitime Shikamoo yaani hiki kijiwe chako ni balaa kinatukumbusha mbali sana sie wengine. Hongera sana sana M/Mungu akupe nguvu zaidi

    ReplyDelete