Wednesday, October 19, 2011

Count down ya nyimbo 50 toka Clouds Radio


Komandoo Hamza Kalala





Clouds Radio imeanza taratibu ya kupiga nyimbo moja kwa kila siku kwa siku 50 hadi kufikia siku ya kilele cha kumbukumbu ya miaka 50  Uhuru wa  nchi yetu. Leo nimeusikia wimbo wa  UDA Jazz Band wana Bayankata. Bendi hii iliyokuwa mali ya shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), usafiri ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya kusafirisha watu katika ya jiji la Dar. Bendi ilipata umaarufu sana katika wakati wake ikiwa na wanamuziki mahiri waliopitia humo kama Freddy Benjamin ambae baadae alikuja kukamilisha maisha yake Vijana Jazz, Maneno Uvuruge mpigaji maarufu wa gitaa ambae kwa wakati huu yuko katika safari USA wakiwa na King Kiki, na pia huko alipitia Komando Hamza Kalala, ambae pamoja na yeye kuwa mwanamuziki mahiri, pia ndie baba mzazi wa wanamuziki maarufu , Kalala Junior na  Totoo Kalala. Hamza Kalala ndiye mtunzi na mpiga solo katika wimbo wa leo katika count down hiyo ya kuelekea siku ya Uhuru. Wimbo huo si mwingine bali ni ule- Tulizaliwa wote. Sehemu ya mashahiri ya wimbo huo ni haya;
Tulizaliwa wote kijiji kimoja,
Lakini ulishindwa kunioa kwa sababu,
Ulisema sina tabia nzuri eeh
Sasa nimeolewa kaka,
Unaanza kuleta chokochoko,
Kujifanya wewe unazo pesa nyingi univurugie.
Wenyewe tumetulia.
Kama ni tabu ni zetu,
Kama unachoringia ni pesa kaka,
Pesa si msingi.
 Chorus
Ninachojali ni utu, pia na heshima kwa mume wangu.

8 comments:

  1. Kaka Balozi. Komando Kalala ni mtunzi mahiri sana katika muziki wa TZ. najiuliza kwa nini TZ tusiwe na tuzo za wanamuziki wa kweli tu peke yake na si kufananishwa na wasanii wa kulazimishwa (fleva). Kwa kweli kuna tofauti kubwa kati ya vipaji na ulazimishaji. TBL leteni tuzo za wanamuziki wetu pekee kwani huu ndo muziki wetu wa asili. Wanamuziki wetu wanahitaji kuenziwa.

    ReplyDelete
  2. seneta wa msondo-usaOctober 20, 2011 at 5:30 AM

    kama ni pesa unachoringia mimi sina haja nazo,ninachojali ni utu pia na heshima kwa mume wangu...aah kaka kitime wanikumbusha mbaaaali commando kalala enzi hizo bwana,mabasi ya uda yale makumba kumba yaliyounganika mara mbili eti tukawa tunayaita mabayankata..kisa mtindo wa bayankata wa uda jazz,raha yake kitime na wewe ungekua unaenda sambamba na hao kina Ruge kwa siku hizo 50 wakiweka wimbo na wewe unauweka hapa tunausikiliza pia.Hivi redio free africa naweza kuipata mtandaoni,wale jamaa nilipokuja bongo nilikuta wana kipindi kizuri sana alhamisi kuanzia saa nne ucku cha muziki wa hizi bendi,yule jamaa mtangazaji anajua sana kupangilia kipindi chake.

    sayz seneta ea msondo,grand rapids,michigan city.

    ReplyDelete
  3. "...usifikiri nimeshasahau ee kashfa na vitendo vyako kijana ee..

    Nachojali nu utu...

    Udaa eee, Bayankata.... Bayankata.

    We acha tu

    ReplyDelete
  4. naona kuna mstari hukuuweka
    unaanza maneno na chokochoko
    kama raha ni matokeo

    ReplyDelete
  5. Wimbo huu unanikumbusha mbali sana. Hamza Kalala ni mwimbaji na mtunzi mahiri. Wapi ninaweza kununua nyimbo hizi?

    ReplyDelete
  6. Mkuu,

    Bayankata bila kumtaja George Mpupua tutakuwa tumekamilisha historia ya Bayankanta?

    Unamkumbuka kulikuwa mzungu anapuliza Trumpet Bayankanta? Halafu walikuwa na Drummer Boy mmoja alikuwa anaitwa Yahaya kama sikosei alikuwa anapiga drums vizuri sana. Huyu jamaa yuko na bendi gani siku hizi?

    Unapanda Bayankanta = UDA likupeleke Paselepa = MWENGE unasepa MLIMANI kuelekea kwa REMMY!

    Mkuu,

    Naomba tuanze mada ya kumbi za muziki wa dansi na bendi zake za enzi hizo. Mimi natoa mtaji wa kuanzia hiyo mada: Msondo wakiwa Amana, Safari Trippers wakiwa Princess, Mlimani Park wakiwa Mlimani, Vijana Jazz wakiwa Vijana Mwananyamala, Marquiz wakiwa Savannah, Makassy akiwa Hunters, Kashama Nkoy wakiwa Kwetu Bar, Matimila wakiwa Lusaka By Night, Biashara Jazz wakiwa Makonde Bar, OSS wakiwa Safari Resort, ZAITA wakiwa Oyster Bay Hotel, Revolutions wakiwa Simba Grill, Barlocks wakiwa Bandari Grill, Bar Keys MountMeru, Les Strocker wakiwa Italian Club/Selander Bridge Club, Super Africa wakiwa Bahari Beach, tuendelee .........

    Weekend njema,

    Mdau Sokomoko Damu, Helsinki, Finland.

    ReplyDelete
  7. hiyo nyimbo ya Uda Jazz ninayo kwenye simu na mara kwa mara huwa naisikiliza...dah ni nzuri mno...

    Bayankata ndio yenyewe

    ReplyDelete
  8. king africa wakiwa mwembeni bar kinondoni kisutu.

    ReplyDelete