Vikao vya matayarisho ya onyesho la mwaka huu la wanamuziki wakongwe vimeanza. Onyesho la mwaka huu ambalo limeonyesha litaweza kupata support zaidi kuliko mwaka jana na hivyo kuwa bora zaidi. Pamoja na onyesho 'live' pia kuna mazoezi makali ya kuweza kutoa album ya nyimbo za zamani zilizopendwa sana kati ya kipindi cha mwaka 1961-1991. Na kwa mwaka huu ni wa 50 kutoka kupata Uhuru 9, Desemba 1961, album hiyo itakuwa ya kwanza katika mlolongo wa album zitakazobeba wazo la miaka 50 ya muziki wa Tanzania.
Mbele King Kiki, nyuma yake Mzee Sangura mpiga bass wa zamani wa Cuban Marimba |
Juma Ubao (King Makusa) na Adinani, mpiga magitaa yote aliyoko Shikamoo Jazz Band |
Waziri Ally(Kissinger) wa Kilimanjaro Band |
Juma Omary(Disco) , mpiga drums wa Kilimanjaro Band |
Mohamed Mrisho (Moddy), mpiga gitaa Kilimanjaro Band |
Mafumu Bilali Bombenga, Saxophone African Beat Band |
Kanku Kelly Trumpetist Kilimanjaro Connection Band |
Yussuph Bernard Saxophonist Mlimani Park Orchestra |
Mabrouk Omary (Babu Njenje), Muimbaji Kilimanjaro Band |
Safi sana, maana inasaidia kuwakumbuka hawa wakongwe, ...tuwaenzi jamani ili kuwapa moyo, wao wamefanya kazi kubwa sana
ReplyDelete