Wednesday, December 22, 2010

Urafiki Jazz Band wana Chakachua 2


Urafiki Jazz Band
Bendi ya Urafiki ikiwa katika hali yake ya uchanga mwaka 1970 ilipata ajali ya gari, wakati kundi zima likitoka katika onyesho huko Chang’ombe, gari lao aina ya Volkswagon Kombi liligonga mti maeneo kona ya Kigogo na Msimbazi Mission.
Baadhi ya wanamuziki waliumia sana na gari lao, likawa halifai kabisa.
Wapigaji walioumia walikuwa ni Hamisi Mashala – Drummer Boy - alivunjika mguu, Mohamed Bakari Churchil aliumia kichwani na kushonwa nyuzi kadhaa, na pia Ayoub Iddi Dhahabu na Maarifa Ramadhani walipata maumivu makali kwa ndani mwilini.

Bendi ilisimamisha maonyesho yake kwa muda hadi  wanamuziki wake walipopata nafuu na kuanza maonyesho tena. Hali ya ajali ile ilileta fikra mbaya kwa wanamuziki hao na wapenzi wao na ilionekana kana kwamba kulikuwa na mkono wa mtu katika ajali ile.  Juma Mrisho ‘Ngulimba’ alitunga wimbo ‘Nimekosa Nini Jama’, wimbo ulioelezea kadhia hiyo. Katika kipindi hiki dhana ya ushirikina ilitawala sana katika bendi mbalimbali. Vifo vya wanamuziki mara nyingi vilihusishwa na upinzani katika bendi. 
Kufikia miaka ya ‘80’ kati bendi ya Urafiki ikawa inasua sua kutokana na uchakavu wa vyombo na Menejimenti iliyokuwepo wakati huo haikuwa tayari kutoa pesa kununulia vyombo vipya. Bendi ya Urafiki ilifikia tamati katika miaka ya ‘80’ kati kati na bendi hiyo ikatoweka katika anga za muziki na kubaki historia.



1 comment:

  1. Balozi, naomba unitaarifu ni wapi naweza kupata nakala za muziki Wa zamani? Mimi Nilikuwa mpenzi sana wa 'Patashika-chakachua.' na ningependa Kujuwa wapi nitapata nyimbo Sao.

    Kingine, naomba nikuulize...hivi ni bendi ipi iliyopiga wimbo Wa 'Mony?'
    ....kiitikio chake: Mony mamaaaa
    Mwimbaji: mwenzio napenda pendo lakooooooo
    Kiitikio: mony mamaaa
    Mwimbaji: oh mony mama njoooooo

    Balozi saidia, nimepata huu wimbo kwenye itune, yaani najiona nimewin kichizi kwani nimenunua albamu yote ambayo ina vijana jazz, Dar inter, sikinde, msondo, nk.

    Ee bongo yangu naipenda!

    ReplyDelete