Friday, December 31, 2010

Boby Farrell wa Boney M afariki dunia


Bobby Farrell, mwimbaji wa kiume katika kundi la  Boney M, amefariki dunia akiwa katika ziara nchini Urusi. Bobby akiwa na umri wa miaka 61 alikutwa amefariki katika chumba chake hotelini huko  St. Petersburg. Bobby aliyefanya onyesho lake Jumatano usiku alienda kulala akilalamika kuwa anajisikia kushindwa kupumua. Asubuhi yake Alhamisi hakuweza kuamka licha ya kujaribu kuamshwa na wafanyakazi wa hoteli hiyo, ndipo mlango wake ulipofunguliwa alikutwa ameshafariki.Kundi la Boney M lilivunjika rasmi 1986.

5 comments:

  1. Urusi nako ni hatari kwa tabia ya kuua watu kimya kima,hapo ni lazima kuna mkono wa mtu au watu.R.I.P.Bobby Farrel.
    Mwanamuziki,Dar.

    ReplyDelete
  2. do you remember da songs like;ELLUTE,MA BAKER BOUNOUNOUS,RASPUTIN,BY THE RIVERS OF BABYLON,RIDE TO AGADIR,CONSUELA BIAZ just to mention a few we used to dance till wewent bananas keep it up brother Kitime,John

    ReplyDelete
  3. Jambo ambalo watu wengi hawafahamu ni kwamba ile sauti nzito ya kiume katika nyimbo za Boney M kama 'Daddy Cool', 'Ma Baker' na 'Baby Do You Wanna Bump' si ya Bobby Farrell bali ni ya mwanzilishi wa kundi hilo ambaye ni producer wa Kijerumani, Frank Farian. Bobby alitumika kwa kiasi kikubwa kama mcheza shoo wa Boney M.

    ReplyDelete
  4. Habari hizi zimenipeleka 1970's jijini DAR ambako kila mahali ulikuwa unasikia nyimbo za Boney M, Abba, Diana Ross, Afro 70 na Mbaraka Mwinshehe. Wasanii wakitangulia mbele ya haki bado wanabaki katika kumbukumbu za waliopenda sanaa zao.

    ReplyDelete