Friday, November 5, 2010

Historia ya muziki Tanzania na maendeleo yake

Mbaraka Mwinshehe na Super Volcano Orchestra




Asiyejua anakotoka ataelewaje anakokwenda? Kuweka kumbukumbu ya muziki wetu na wanamuziki wetu wa zamani ni muhimu katika kuweza kujitafuta wenyewe kimuziki. Bado naona kuna tatizo la baadhi ya  wanamuziki wa Tanzania kupata utambulisho wa Utanzania kwa kuwa hawana uhusiano kati ya muziki wao wanaoupiga,  na aina yoyote ya muziki wa awali wa Tanzania. Nikisema muziki hapa nina maana ya aina zote za muziki, wa kiasili, Taarab, dansi na kadhalika. Katika nchi moja wapo ya Ulaya ya Mashariki baada ya kuona uhuru mpya umewezesha mfumuko wa vyombo vya utangazaji ambavyo vyote vikaonekana kuupa mgongo muziki wa zamani wa nchi hiyo, serikali imeweka amri inayolazimisha asilimia 10 ya muziki unaopigwa na vyombo hivyo kuwa ni muziki wa zamani wa nchi hiyo. Matokeo yake vijana wa nchi hiyo wameanza kutunga muziki wakitumia hazina hiyo na kuweza kujitokeza kuwa ni tofauti na wenzao wa nchi jirani. Jaribu kusikiliza muziki mpya wa Tanzania pamoja na kutungwa mashahiri mazuri yenye hadithi za Kitanzania , muziki unaopigwa hauna uhusiano na muziki wa Kitanzania, aidha unaiga Kwaito au Soukus, zouk au moja kwa moja Rock and Blues toka magharibi na kadhalika. Wale wachache wanaoanza kutumia muziki asili, kama mdundiko mchiriku, na kadhalika wanajikuta wananyimwa nafasi ya kusikika. Kuiga huku mitindo iliyomaarufu hurahisisha kuuza kazi hapa nchini, lakini kazi hizo hazichukuliwi kwa uzito wowote katika anga za wasambazaji wa kimataifa. 

17 comments:

  1. Hii inafaa itumike na hapa. Kuna kipindi watoto wa wanamziku kama akina Braka mwishehe walianza kuzipiga upya nyimbo za baba zao kama sikosei, nafikiri nyimbo hizo zikipigwa upya na `kuigizwa' inawezekana tukalinda hazina hiyo nzuri!
    Ni wazo tu

    ReplyDelete
  2. SUALA LA KUUPENDELEA MUZIKI WETU WA NA KUUPA ASILIMIA FULANI KTK AIR TIME NI MUHIMU SANA,LA SIVYO KTK SIKU ZA USONI NI KWELI TUTAPOTEZA KILA KITU,SABABU VIJANA NA WATOTO,MUZIKI WANAOUSIKIA NDIO WANAOJIFUNZA.ITABIDI TUFANYE KILA NJIA NA SISI TUWE NA SHERIA ITAKAYOSHINIKIZA ASLIMIA FULANI YA AIR TIME KWENYE MUZIKI WETU.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  3. Bwana Kitime,swala la muziki wa Tanzania au wenye vionjo vya kitanzania,inahitaji uzefu nakipaji cha hali ya juu ili uwe na muziki wenye mfanano wa hicho unacho kisema.polelepole tutafika,
    kaka s

    ReplyDelete
  4. Awali Radio Tanzania Dar-es-salaam (RTD), na pia siku za wali za TBC_Taifa walikuwa wanazienzi saaana nyimbo zetu zamani. lakini kwa mshangao sijui waliathirika kivipi wakaondoa muziki wetu na ulikuwa ukisikiliza kwa siku nzima nadra sana kuona nyimbo za zamani zikipigwa. RTD alikuwa mkombozi kweli kweli sielewi mdudu gani amewaingila

    ReplyDelete
  5. Nimepata taarifa kuwa ni agizo limetolewa muziki huo usipewe kipaumbele

    ReplyDelete
  6. Suala nilionavyo mimi ni wanamuziki wenyewe kuleta mapinduzi makubwa; vinginenyo malalamiko hayataisha. Na njia ni nyepesi kuanza kufanya matamasha (concerts). Na kama nia ni njema basi wanamuziki waondoe tofauti zao na lengo liwe moja tu kuuzundua muziki wetu wa asili ambao umelala. Matamasha hayo yawe programed katika hali kwamba yasiishie Dar-es-salaam tu bali hata mikoani. Najua kikwazo itakuwa wadhamini. lakini tukijipanga sawa yanawezekana

    ReplyDelete
  7. Kama ni kweli kuna agizo linaloitaka TBC inachane na muziki wa zamani, basi hakuna haja ya taasisi hiyo kuendelea kuwepo. Ikumbukwe kuwa hii ni redio ya taifa na haipaswi kujishusha hadhi na kuwa kama utitiri wa vijistesheni vya FM ambavyo havitoi mchango wowote katika kuuenzi muziki wa Tanzania. Napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Radio Free Africa kwa kuendelea kuuenzi muziki wa kweli wa Tanzania.

    ReplyDelete
  8. Ni kweli Radio Free Africa inatoa mchango mkubwa sana kwetu wapenzi wa muziki huu, ni raha sana, siku za Alhamisi usiku huwa nazima TV na sitoki ni kuburudika na Radio Free Africa

    ReplyDelete
  9. Ni wajibu wetu kuhuisha urithi wetu kama Waafrika na Watanzania. Kuna baadhi ya vituo vya TV na redio vinafanya kazi hii; lakini vituo vingi vimelala. Inasikitisha kuona Tv station kama vile EATV wanaonyesha video za hip hop na za kizungu kwa kiasi cha 90%!!!! Let's emancipate ourselves from mental slavery...none but ourselves can free our minds...

    ReplyDelete
  10. Ningelikuwa na uwezo ningelitenga siku ya muziki wa zamani tu Tanzania na kuamuru siku nzima redio zipige nyimbo na kueleza historia ya wanamuziki na bendi za zamani akiwemo Mbaraka. Sasa kwa kweli radio free wanajitahidi sana hata mimi huwa sipitwi tena tuna mpango wa kuanzisha club yetu ya kusikiliza musiki wa zamani kila week end. Zamani Nilipata kusikia kuwa Mbaraka alianzia muziki alipokuwa akisoma Mzumbe Sekondari sijui kama ni kweli nilijaribu kufuatilia nilipokuwa nikisoma pale lakini sikupata habari za kuaminika. Msaada kwa hilo tafadhali wadau.

    ReplyDelete
  11. Uncle Kitine na wadau wengine ntaomba wachangie kwa hili. ningependa kam itawezekana uweke ratiba za bendi za zamani ambazo zinaendelea kupiga has hapa Dar tafadhali nakosa ladha ya live music.

    ReplyDelete
  12. KAMA KUNA AGIZO LIMETOLEWA KUUA MUZIKI WETU JIBU NI RAHISI TU,NI KUTOA USHIRIKIANO NA KUWA PAMOJA NA REDIO CHACHE ZINAZOBEBA MUZIKI WETU.NA MATAMASHA NI MUHIMU KAMA ALIVYOSEMA MDAU MWENZANGU.WADHAMINI WATAPATIKANA TU.TUKIWA NA USHIRIKIANO SISI KWA SISI TUTASHINDA.

    ReplyDelete
  13. Nimepata taarifa kuwa mwanamuziki Numbi Kileba 'Vicky' amefariki dunia jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Novemba 4, mwaka huu. Huyu namkumbuka sana enzi za Ndekule katikati ya miaka ya 80, hasa katika kibao 'Shukrani kwa Mjomba'. RIP Vicky.

    ReplyDelete
  14. mimi naomba sime kitu hapa kwamba Muziki hauna hauna utaifa bali ni sanaa,ambayo mtu anajifunza kwa kuiga au kusoma,ni kwamba muziki kila mtu alieanza anafuata kazi za mtu mwingine na baadae anakua na kitambulisho chake kimuziki!leo mnasema watu wanapiga soukous hata nyinyi kina kitime mlikua mkipiga Rhumba la kutoka huko huko Congo kwa kiwango chenu.Nakubaliana kabisa na nyinyi kwamba Muziki unaopigwa na Bandi za TZ haupingwi sana kwenye Radio nyingi kwakua kunaufisadi mwingi sana kwenye hizo Radio.kwamba mziki kupigwa mpaka utoe rushwa.Ni ni hawa vijana wa kisasa ndio walokuja na mambo hayo kwani wengi wao ndio walioajiriwa na hizo Radio tunategemea nini??Sikubaliani na wewe Kitime kwamba mnavyokua mnadai kwamba nyinyi wazamani pekee ndio mliokua mkipiga mziki mzuri na wa kitanzania.wanamuziki wengi tu wapo wanapiga Muziki kuwazidi ila ndio hivyo Rushwa inatuumiza!wakati wenu kulikua hakuna Bongo fleva na huko Radioni kulikua na watu wa kizazi chenu na wenye kufuata maadili!

    ReplyDelete
  15. Waafrika Magharibi wanatushinda sana katika kuenzi staili zao mpaka vyombo vyao vya asili ambavyo huvitumia sana kwenye miziki yao hata iitwayo ya kisasa. Hili pia huwasaidia sana kuuza sanaa yao nje kwa kuwa muziki wao huonekana tofauti.

    Sasa sisi na BONGO FLEVA zetu ni vigumu sana kuuza nje kwa kuwa watu huzifananisha na HIP HOP ya Marekani na jibu liko wazi kuwa kama unaweza kumuona JAY Z na akina Kanye WEST ni vigumu kufikiria kuweka HIP HOP ya BONGO kwenye soko kirahisi ambayo itakuwa inagombea soko hilo hilo lililotawaliwa na Wamarekani.


    R.I.P Numbi Kileba!

    ReplyDelete
  16. yaani ukilinganisha muziki wa leo na wa zamani kuna tofauti kubwa sana. arrangement of instruments and the music itself iko very superior. Computer haikua mwanamuziki zama hizo. Kila instrument ilipigwa na talented musician na waimbaji walikua na sauti safi sana. nikisikiliza wimbo naweza kutambua kila mwimbaji kwa sauti yake. It was very well done. Bado nina casette ambazo nilinunua zaidi ya miaka 15 zilizopita. Nashukuru Kitime kwa update zako.

    ReplyDelete