Monday, October 4, 2010

Intimate Rhumba

Mwishoni mwa miaka ya themanini, lilitengenezwa kundi lililokusanya wanamuziki mahiri wa Kitanzania na Kikongo na kuunda bendi iliyoitwa Intimate Rhumba, kundi hili halikukaa muda mrefu wala halikuweza kurekodi. Baadhi ya wanamuziki waliokuwemo katika kundi hili wanaimani kuwa  bendi yao iliuwawa kwa kutumia uchawi. Wana amini walionekana ni tishio mno kwa kundi lililokuwa na ukaribu nao la Ndekule na hivyo kufanyiwa ulozi na kuvunjika. Pichani ni Intimate Rhumba wakiwa jukwaani kati yao wa kwanza kushoto Mawazo Hunja, watatu Kabeya Badu, King Kiki, mwisho na Joseph Mulenga

4 comments:

  1. Kitime,nalikumbuka hili kundi lakini miaka yote nilikuwa najua ni bendi B ya OSS, hasa kutokana na kuwepo kwa King Kiki na Kabeya Badu, na hata mavazi yalikuwa yakifanana na yale ya Ndekule pamoja na Mlimani

    ReplyDelete
  2. kwenye hiyo baada ya Mawazo Hunja ni marehemu Ngoyi Mubenga, kabeya, King Kiki, Vickii na Mulenga. Nani alikuwa mmiliki wa bendi hii, mimi nilidhani ni Hugo Kisima

    ReplyDelete
  3. Bendi hii ilikuwa chini ya mke wa Hugo Kisima, ilionekana inapendelewa kwani pamoja na ugeni wake , ilikuwa ikipata hata mishahara kabla ya OSS, na hivyo kuanza kuleta uhasama wa chinichini.

    ReplyDelete
  4. uncle kitime ukumbi kama silent inn hapo

    ReplyDelete