Monday, July 30, 2012

Enzi ya Dansi la Buggy



The Rifters
The Flaming Stars
Utamaduni wa Buggy ulitamba sana katika miaka ya 60 na70. Buggy lilikuwa ni lile dansi la mchana la vijana. Kutokana na malezi ya wakati ule, wanafunzi hata kama ni wa sekondari ilikuwa marufuku kuhudhuria madansi ya saa nane za usiku. Hivyo basi ili kukidhi haja ya vijana kupata muziki wao na kupiga muziki wao, kulikuweko na utamaduni wa Bugi. Dansi la bugi lilikuwa likianza mara nyingi majira ya saa nane mchane na hata kabla ya hapo, dansi hili liliendelea hadi saa 12 jioni na mara chache kufika saa moja usiku, ambapo vijana walikimbia haraka nyumbani kabla giza halijaingia, Maafisa Utamaduni walikuwa wakiweza kufungia bendi yenye kibali cha Bugi kuzidisha muda na kuendelea na dansi baada ya saa moja usiku. 
Shule nyingi hasa za sekondari zilikuwa na bendi, na hata shule nyingine zikiwa na bendi zaidi ya moja, kulikuweko na bendi za vijana kutoka mitaa mbalimbali zikiwa na ushindani mkubwa wa kupiga nyimbo zilizokuwa zikitamba katika mabara ya Ulaya na Marikani, vikundi hivi ambavyo leo tunaweza kuvilinganisha na vikundi vya sasa vya  wanamuziki wa Bongoflava, pia vilikuwa na majina ya bendi maarufu zilizotamba Ulaya na Marekani wakati wakati huo, kulikuweko na mjina kama The Flames, The Flaming Stars, The Sparks, The Experience, Crimson Rage, Black Beatles, The JBs, na kadhalika. Kutoka katika bendi hizi kukatoka makundi ya kihistoria kama vile Safari Trippers, Afro 70, Tanzanites awali Barkeys, Kilimanjaro Band awali The Revolutions, na kadhalika. Bahati mbaya sana utaratibu huu ulipigwa breki baada ya kiongozi mmoja wa kisiasa kupiga marufuku Bugi, kuna hadithi kuwa alipiga marufuku taratibu hiyo baada ya binti yake kulala siku kadhaa nyumbani kwa mwanamuziki mmoja. Lakini kwa vyovyote vile pengo lililotengenezwa halitazibika, kwani iliwaondoa wanamuziki wa Tanzania katika safari ya muziki ambayo nchi nyingine Afrika zilikuwa zinafanya, pengo lililotokana na amri hii halijaweza kujazwa mpaka leo.

1 comment:

  1. I remember those BOOGIE Days! It was sheer heaven on earth. Weekdays were for studying hard, and engaging in sports; and weekends were for the party-hearty of the boogie-woogie, involving the Shingaling, etc etc. Wow, those were the days! Shame on the damn politician who banned boogies. He should have sanctioned his daughter, ie stopped her from attending boogies, and NOT punished all other innocent and responsible youth who were having some HARMLESS fun, within decent time limits for students.

    SAFARI TRIPPERS and RIFTERS were my favourite bands, among a few others.

    Man-oh-man~ those were the days!

    ReplyDelete