Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka
maarufu kwa jina la Bi Kidude
amefariki dunia muda mchache uliopita huko Bububu Zanzibar, sehemu alikokuwa
anaugulia kwa kipindi sasa. Mwili wake utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi
yatakuwa kesho. Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo, alikuwa
binti wa mchuuzi wa nazi, hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe
ngapi, kuna hata mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102.
Katika mwaka
1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao,
mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka
miji mingi ya Tanganyika wakati ule , mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali
alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.
Bi Kidude pia liwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa
ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote
akiimba katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni
Mungu Amlaze Pema Peponi Bibi yetu. Amen
No comments:
Post a Comment