KONYAGI KUIKABIDHI MSONDO VYOMBO IPYA IJUMAA HII LEADERS CLUB
Katika habari nzuri kwa muziki wa dansi wiki hii ni sherehe ya Msondo
Ngoma kukabidhiwa vyombo vipya na kampuni ya Konyagi siku ya Ijumaa pale
Leaders Club. Kupatikana kwa vyombo hivyo kutaleta burudani zaidi na
changamoto kubwa katika muziki wa dansi Tanzania. Msondo, ambayo ni moja
ya bendi za zamani kuliko zote nchini Tanzania imejiwekea heshima ya
kuwa ikienda na wakati na hivyo kuweza kuwa na wapenzi nchi nzima na
hata nchi jirani, katika uhai wote wa bendi hii.
No comments:
Post a Comment