Kwanza kabla ya kuendelea na historia hii ya Simba wa Nyika na matawi yake lazima nitoe shukrani za dhati kwa mwanamuziki Abou Omari Njenga, ambaye bila yeye historia hii tusingeipata. Abou ambaye kwa sasa anaishi na kupiga muziki Japan, pia alipitia na kupiga katika makundi haya ameweza kukusanya karibu yote ninayoyaandika humu. Kwa kuwa naye pia likuwa mmoja wa wanamuziki wa makundi haya tutasikia habari zake katika maendeleo ya simulizi hii. Aksante sana Abou.
Wimbo wa ‘Sina makosa’ kwa kweli ulikuwa kama wimbo wa Taifa wa Afrika Mashariki, kila ulipoenda uliusikia na mpaka leo bendi nyingi zinaendelea kuupiga wimbo huu mzuri. Wimbo huu ulitungwa na Profesa Omari Shaabani ambaye ndiye aliyekuwa mpiga gitaa la rhythm na Kiongozi wa Les Wanyika. Muimbaji kiongozi katika wimbo huu alikuwa Issa Juma, waliokuwa wakijibu walikuwa John Ngereza ambaye pia alikuwa akipiga solo na Mohamed Tika. Huyu John Ngereza, ambaye alitokea Amboni Jazz Band ya huko Tanga, aliendelea kuimba na kuwa muimbaji mzuri na anasikika vizuri katika nyimbo kama Afro, Amigo na Nimaru. Issa Juma sauti yake iliongoza nyimbo kama vile Pamela, Paulina, Kasuku na Usia wa Baba. Profesa Omari Shaaban mtunzi wa 'Sina Makosa' |
No comments:
Post a Comment