Thursday, March 1, 2012

Alikotokea Marehemu Jerry Nashon aka Dudumizi


Jerry Nashon
Jerry Nashon alikulia katika  kijiji kiitwacho Kigera kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma jirani na shule ya Sekondari Mara. Jerry alianza kujifunza gitaa akiwa Musoma Catholic Mission club ambayo leo ni Mwembeni secondary School. Alikuwa ana mazoea ya kwenda kwenye hiyo social club ya kanisa iliyofanya kazi nzuri sana ya kuwaunganisha vijana wenye vipaji mbalimbali. Alijiunga katika bendi ya Special Baruti Band iliyokuwa na Rashid Ruyembe  mwaka 1980. Jerry alianza kuendelezwa na Charles Koya ambaye wakati huo alikuwa mpiga rhythm wa bendi hiyo. Alikuwa mwanafunzi mzuri na baada ya muda mfupi alikuwa mpigaji mahiri na akaweza kurekodi na  bendi yake hiyo katika studio za Tanzania Film Company, RTD na hatimaye katika studio mbalimbali nchini Kenya. Jerry na Special Baruti Band walifanya maonyesho mengi katika jiji la Nairobi , katika kumbi na club mbalimbali kama vile Bombax Hotel, Kaka Night Club, Rwadhia Night Club na nje ya Jiji katika mikoa takribani yote ya Kenya kasoro Mombasa na Kisumu. Katika kumwona kiongozi wa bendi hiyo, ambaye ndiye alikuwa mtunzi na mwimbaji akipata umaarufu mkubwa nae akaona heri ahame kutoka upigaji wa rhythm na kuwa mwimbaji mtunzi. Taratibu alianza kujifunza na juhudi zake zikaonekana na Jeshi la Magereza  Musoma nalo likamchukua akajiunge na Magereza Jazz Band. Baada ya miaka miwili na nusu hivi akiwa na Special Baruti Band Jerry alihamia Dar es Salaam. Wakati huo mji wa Musoma ulikuwa na bendi nyingine, kulikuweko na Musoma Jazz Band waliopiga kwa mtindo wao wa Segese, Mara Jazz Band maarufu kwa mtindo wao wa Sensera, pia ilikuwepo bendi iliyomilikiwa na  Seminary ya Kikatoliki ya Makoko, hii iliitwa Juja Jazz band , haikuwa na mtizamo wa kibiashara hivyo haikuwa na umaarufu kama zilizotajwa hapo juu. Jerry alidumu kwa muda Magereza Jazz band kasha akahamia Bima Orchestra nahatimae  Vijana Jazz Band mpaka mauti yake.


8 comments:

  1. Nyasaye achiel merwa kende, an aheri 'makulata, nyar pacho ibi mak lweta itera mbele ya wazee!!!!

    Dah acha kabisa kipande iyo!

    ReplyDelete
  2. Sahihisho. Jerry Nashon alikuwa na Vijana Jazz kwa takriban mwaka mmoja na nusu kabla ya kuhamia Bima Lee 'Magnet Tingisha' mwaka 1983. Ikumbukwe kuwa Bima Lee hiyo iliyosukwa upya pia ilikuwa na wanamuziki wengine waliokuwa na majina makubwa enzi hizo kama Shaaban Dede, Joseph Mulenga (RIP), Athumani Momba (RIP) na Suleiman Mwanyiro (RIP). Huko walikutana na wanamuziki wengine wa Bima Lee kama Rweyemamu 'Roy' Bashekanako na Jumbe Ahmad Omar Jumbe (J.A.O. Jumbe) ambao kwa pamoja waliifanya Magnet Tingisha kuwa ni moto wa kuotea mbali. Nashon alirejea Vijana Jazz mwanzoni mwa miaka ya 90 baada ya kifo cha Hemed Maneti.

    ReplyDelete
  3. Kweli, nakumbuka jerry alitoka Vijana then Yeye pamoja na Momba na wanamuziki wengine wakaenda Bima baada ya kulalamika kuwa uongozi wa Maneti ulikuwa mbovu. Wanamuziki wengi wa Vijana walihama kipindi kile na kuunda Bima mpya ya magnet Tingisha na huku Vijana ikaundwa upya na kuitwa Pamba Moto awatu ya pili. Duh Bongo kipindi hiki muziki ulikuwa mtamu saana. Bima, Vijana, msondo, Nginde, Super Rainbow chini ya marehemu Sheggy, na Kimulimuli chini ya Zoro....ah Tanzania nchi yangu pole sana kuwa kuna watu wanafanya mapinduzi ya nguvu kuua utamaduni wako na kukulazimisha/kukuletea vitu vya watu wa nje alsonabl stUNatihuku wakibatiza kuwa ni vyako kumbe wanajidanganya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tanzania yangu imepoteza kabisa hazina iliyoipa nchi sura halisi (identity). Kilichoingia sasa ni aibu tupu kama si upuuzi.

      Delete
    2. kweli kabisa mimi nilishabikia RTD.utotoni mwangu nikiwa Kenya,
      Muziki mtamu ajabu

      Delete
  4. Jerry Nashon: Nimesimama chini ya Mnara wa ...bara bara kubwa iendayo bandari ya Salama mawazo yamenijaa machozi yanimwagika naiwaza sura ya Neema naiwaza sura ya malaika wangu he heh he eh!


    Kibwagizo: Umenikataa sababu mimi ni...mkono wangu haunyooki eti nina mkono wa birika mamaaa:

    Kibwagizo : Nitoe nitoe kiizimbani niwe huru mtoto wa Songea! Nitoe nitoe Kiizimbani niwe huru eh niwe huru

    Kibwagizo :"Usiniache peeke ..Neema Nitapendwa na nani mama Usifate wayasemayo wafitini wao wapo mbele mbele kuharibu mapenzi yetu mimi nawe."

    Jerry Nashon: "Maneno mengi sana yalishasemwa.. Usifate ya wambea watakuja kutuvurugia unawaona mama ... Tumependana kweli ... Tumepeendena bado tuna pendana Neema mama"

    Mwanamuziki " Nilipopokea ahadi uliyonipaa aaah! Umeniacha pekee sina mwingine ....... (Kiitikio) Sina mwingine Neema eeeh !Fanya hiima"


    MAGNETOOO ! TINGISHA....MAGNETOOO...TINGISHA

    vipande vingine nimevisahau .

    ReplyDelete
  5. Jerry na dede walifanya kazi nzuri sana bima kwa kushirikiana na kina momba,kila wakati nimekua nikimshawishi dede ajaribu kuzirudia nyimbo alizotunga akiwa bima ile amekua akiniahidi kufanya hivyo tatizo sponsor.

    Jerry kwangu ni mmoja wa wanamuziki bora kabisa kupata kutokea bongo.

    Badi bakule alikua ananikumbusha sana jerry kwa jinsi alivyokua akiiga sauti yake na kukiri kwamba jerry alikua role model wake,safi sana hii kuona wazee wanaacha alama

    seneta wa msondo,revere,masachussetts,usa

    ReplyDelete
  6. Kweli Seneta wa Msondo. Line-up ya uimbaji ya Shaaban Dede, Jerry Nashon na Athumani Momba katika Bima Lee ilikuwa ni balaa.

    ReplyDelete