Wednesday, October 12, 2011

Patrick Balisidya akiwa jukwaani akiimba utabiri wake?

Patrick anaimba wimbo ambao aliupiga kwanza akiwa na Afro70. Wimbo huu una ukweli mkubwa, unakufanya hata ufikirie kuhusu Patrick mwenyewe, kweli wema hawana maisha. Hapa Balisdya akiwa jukwaani na Shikamoo jazz. Mzee Zahoro anaonekana hapa akipiga mandolin chombo ambacho amepiga sana hasa akiwa Kiko Kids. Tunaambiwa wakati bendi zote Tabora zilianza kutumia magitaa ya umeme yeye akiwa na kiko Kids yake aliendelea kutumia Mandoline na ndio husikika katika nyimbo zake za zamani za Kiko.

No comments:

Post a Comment