Saturday, October 22, 2011

Freddy Supreme--Ndala Kasheba


Leo tunatimiza miaka saba toka kifo cha mwanamuziki mahiri Ndala Kasheba. Freddy Supreme au maarufu kwa wengi kama Ndala Kasheba alianza kujifunza gitaa akiwa na umri mdogo wa miaka 12, alipofika umri wa miaka 17 alikuwa tayari mwanamuziki mahiri wa Orchestre Fauvette, akiwa na wanamuziki wenzie kama Baziano Bweti na King Kiki. Mwaka 1968, kundi zima la watu tisa lilipanda mashua za walanguzi wa chumvi na kuvuka Ziwa Tanganyika toka Kongo hadi Tanzania kwa kupitia Kigoma. Kundi hili, Fauvette lilitikisa anga za  Tanzania kwa vibao ambavyo wengi huvikumbuka mpaka leo, kama vile Fransisca, Vivi, Nono na Kalemie, Zula, Jacqueline. Kasheba aliweza kuimarisha jina lake zaidi alipolifanya maarufu gitaa la nyuzi kumi na mbili, mwenyewe akiliita nyuzi dazani, hasa alipoanza kulipiga kwa mtindo wa Dukuduku akiwa Safari Sound Orchestra. Pamoja na bendi hizo Kasheba pia alipitia  Safari Nkoy, Zaita Muzika, Kasheba group, pia alipita Maquis, na kwa wiki chache alipitia Tancut Almasi.
Kasheba alifariki 22 Oktoba 2004 akiwa na miaka 58.
                                                   Mungu amlaze pema peponi Amen

2 comments:

  1. Nitapata wapi cd zilizo katika ubora za OSS dukuduku pamoja na za wakati wa masantula?

    ReplyDelete
  2. Bwana Kitime, nakushukuru tena kwa dhati kwa kazi yako maarufu ya kutukumbusha juu ya miamba yetu iliyopita ya muziki wa nyumbani. Hivi nakuuliza, je unaweza kupost video za Maestro wakati walikuwa Maquis, pamoja na King Kiki, Chinyama na wengineo? Pia naomba tafadhali ikiwa una video ya Mbaraka Mwinshehe utuandalie hapahapa. Shukrani

    ReplyDelete