Mzee Morris Nyunyusa |
Kwa miaka nenda rudi wengi tulikuwa tukisikia midundo ya ngoma iliyokuwa inaashiria kuanza kwa taarifa ya habari katika redio ya Taifa, toka enzi za TBC hadi RTD. Ngoma hizo zilipigwa na mwanamuziki aliyekuwa na ulemavu wa macho si mwingine bali ni Mzee Morris Nyunyusa. Pamoja na kutokuwa na uwezo wa kuona Mzee huyu alikuwa anaweza kupiga ngoma 17. Kwa bahati mbaya sana ngoma hizo hazisikiki tena katika redio zetu lakini ujuzi wa Mzee huyu bado haujafikiwa na wasanii wa leo.
No comments:
Post a Comment